Monday 26 December 2011

NDIKUMANA AMTOROSHA MWANAE


 
NA IMELDA MTEMA
MSANII ‘hot’ wa filamu Bongo, Irene Uwoya amejikuta akisherehekea Sikukuu ya Chrismasi kwa machungu kufuatia mumewe Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kutoweka na mtoto wao Krish katika mazingira ya kutatanisha.
Akizungumza kwa njia ya simu na Ijumaa Wikienda Jumamosi ya Desemba 24, mwaka huu, Irene alisema mpaka siku hiyo alikuwa hajui aliko Ndikumana na mtoto wao, hali iliyomfanya achanganyikiwe.
Alisema: “Mimi na Ndikumana tunakaa Sinza, jana asubuhi (Ijumaa iliyopita) yeye (Ndikumana) aliamua kwenda kumuangalia mtoto ambaye siku zote anakaa na bibi yake huko Mbezi.
“Alipofika alimkuta msichana wa kazi, mama hakuwepo, yule msichana akamuachia mtoto na kwenda gengeni, hapo ndipo Ndikumana alipoondoka na mtoto na kuanzia siku hiyo hakurejea Mbezi wala Sinza,” alisema Uwoya kwa masikitiko.
Akaendelea kueleza kuwa, kufuatia hali hiyo alianza kuwasiliana na Ndikumana ili kujua aliko lakini matokeo yake aliambulia meseji za vitisho.
“Nilipojaribu kumtafuta kupitia simu yake ili kujua aliko alianza kunitumia meseji za vitisho tena mbaya zaidi vilikuwa vitisho juu ya mtoto, kwa kweli amenichanganya sana.”
“Hata kama tunagombana mara kwa mara lakini kitendo cha kutoroka na mtoto kisha kunitumia meseji za vitisho siyo sahihi na kwa kweli siwezi kukivumilia, nimempa saa 24 amrudishe mtoto laa sivyo nitamchukulia hatua za kisheria,” alisema Uwoya.
Mpaka gazeti hili linakwenda mtamboni, jitihada za Ndikumana kupatikana zilikuwa hazijazaa matunda na ikaelezwa kuwa Uwoya alikuwa katika jitihada za kufungua jalada la kesi kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

toka GPL

1 comment:

  1. too much drama hata lindsay lohan na rihanna wanaiga.hovyoooooooooooooo wote mtu na mkewe!!

    ReplyDelete