Tuesday 6 December 2011

WEMA,WOLPER WAPARURANA MAKUCHA LIVE KUMGOMBEA DIAMOND





VITA imezidi kukolea na sura iliyopo inaonesha kuwa Mastaa wa Filamu Bongo, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper wanaweza kudhuriana baada ya kuparuana kwa ugomvi ambao kama si busara za wengine, leo hii habari ingekuwa nyingine.

Ilishaelezwa kuwa warembo hao wana ‘bifu’ la muda mrefu ambalo chanzo chake ni penzi la brazameni wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Jumapili iliyopita, Wema na Wolper walivaana kisharishari kila mmoja akiapa kumshikisha adabu mwenzake lakini waungwana wakawaamua kabla mambo hayajawa mabaya zaidi.

Dalili za hatari na umwagaji wa damu zilishaonekana, kwani kuna watu walijigawa pande mbili, wapo waliomsapoti Wema na wengine Wolper.

Kutokana na tifutifu hilo, chupa za bia ambazo ilidaiwa zilitoka upande wa Wolper, zilirushwa na kumkosa Wema kwa umbali wa sentimita chache.

CHANZO CHA UGOMVI
Diamond kwa sasa ni mchumba wa Wema lakini kabla ya kuanza kutoka na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006-07, alifungua ukurasa na Wolper.

Siku ya tukio, wasanii kibao wa Bongo Movie wakiwemo Wolper na Wema, walikuwa wanasherehea siku ya kuzaliwa ya kaka mkubwa wa tasnia hiyo, Jacob Steven ‘JB’, ndani ya Viwanja vya Leaders Club.

Milango ya saa tano usiku, sherehe ilipambwa na ngoma ya Diamond ‘Moyo Wangu’, ghafla Wolper akaanza kuicheza huku akitamba: “Ooh mume wangu huyo!”

Madai ni kwamba tambo na mijishauo ya Wolper ilimfikia Wema ambaye alimvaa mwana-filamu mwenzake huyo na kumchimba ‘kibesi’ kama ifuatavyo:

Wema: Wewe … (lugha kali), kwa nini unamshobokea mume wangu?

Wolper: Mume atakuwa Diamond? Kwanza mtu mwenyewe ana … (lugha kali).

Wema: Sawa hata kama ana … (lugha kali) si ni wangu? Wewe yalikushinda, nimemsafisha na kumtunza mwenyewe ndiyo unaanza kumshobokea.
Baada kujibishana hayo, kila mtu alishika hamsini zake.

WOLPER AKALIENDELEZA
Inadaiwa kuwa baada ya kila mmoja kumpotezea mwenzake, Wolper alianza kupita meza moja hadi nyingine akimponda Wema ambaye alipopata taarifa, akaamua “kama noma na iwe noma tena ikibidi ile kinoma.”

Katika hatua hiyo, The 5Star Paper, Risasi Mchanganyiko, lilishuhudia kipindi cha “tusi nikutusi” kati ya Wema na Wolper.

Hata hivyo, baadaye mambo yalipokuwa mabaya, Wema alimfuata mlezi wa wasanii wa filamu, Husna Posh ‘Dotnata’ na kumlalamikia kuhusu tabia ya Wolper.

Jitihada za Dotnata na wahudhuriaji wengine wastaarabu, waliweza kumaliza mtiti huo, ingawa wapo mashambenga waliokuwa wanashangilia huku wakiombea ndondi zipigwe ajulikane nani mkali.

BUSARA ZA DOTNATA
Dotnata alipozungumza na gazeti hili, alisema: “Mimi niliona si busara kuwaacha wagombane mbele ya watu kwani siyo vizuri. Kwangu mimi, wale wote ni wanangu, hivyo sipendi wagombane.”


 NENO LA WEMA
Staa huyo wa filamu alisema: “Yule (Wolper) simuelewi.

Aliwahi kutoka na Diamond wakaachana. Akamkashifu kwa maneno mengi akasema ana … (lugha kali). Sasa hivi anaanza kumtaka. Mara nyingi nimenasa meseji zake nyingi kwenye simu ya Diamond akimtaka, halafu leo anataka ugomvi na mimi, yeye kaja kutafuta maisha Dar, mimi kanikuta hapa, hana class (kiwango) ya kugombana na mimi kabisa.”

HUYU NI WOLPER
Wolper alipoulizwa na paparazi wetu kuhusu ishu hiyo, alitamka: “Mimi nimtake Diamond? Mtu mwenyewe ni … (lugha kali). Yule hawezi kuingia hapa kwangu.
Na huyo Wema kama anataka ugomvi, ajiandae, asidhani mimi ni mtoto wa mama mwenzake.”

ZE SAGA KONTINYU
Sakata linaendelea, kwani hivi karibuni, gazeti ndugu na hili, Amani liliandika habari ya Wema na Wolper kuingia kwenye tifu zito, chanzo kikiwa ni lile lile penzi la Diamond.

Katika habari iliyoandikwa na Amani, ilielezwa kuwa Wema na Wolper walikuwa wanapakana mbovu kupitia ukurasa wa watumiaji wa simu za Blackberry (BBM).

toka:gpl

No comments:

Post a Comment