Sunday, 11 December 2011

RAY ATANGAZA BIFU NA ZAMARADI

BUSINESS icon kunako tasnia ya filamu za Kibongo, Vincent Honorat Kigosi ‘Ray’ ametangaza rasmi kuingia kwenye bifu zito na mtemea ‘maiki’ wa kipindi cha Take-One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema kwa madai kuwa amechoka kupondwa redioni na mwanadada huyo.

Akizungumza mbele ya The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda huku Zamaradi akisikilizia ‘beto’, Ray alimpa kavukavu kuwa siku zote amekuwa akiishi kwa kumvumilia mtangazaji huyo kutokana na tabia yake ya kumchafua kwa kuponda kazi zake za filamu kila uchwao.

Kwa mantiki hiyo, Ray alitangaza bifu la maisha na Zamaradi akiweka wazi kuwa haogopi chochote kwani maisha yake hayamtegemei mtangazaji huyo.

IJUMAA WIKIENDA USO KWA USO NA RAY
Baada ya kusikia maneno mazito (mengine hayaandikiki gazetini) yakitoka kwenye kinywa cha Ray, Ijumaa Wikienda lilimvuta pembeni mwigizaji huyo ili afunguke kwa mapana juu ya bifu lake na Zamaradi ambapo alisema kwa muda mrefu mwanadada huyo amekuwa akimchafua licha ya jitihada za kukutana naye na kumuomba msamaha kama alikuwa amemkosea jambo, lakini aliendelea kumchafua.

ZAMARADI ANASEMAJE?
Ulifika muda wa Zamaradi ambaye muda wote alikuwa kinywa wazi kwa mshangao ambapo alifunguka:
“Umesikia mwenyewe alichosema na si wewe tu, kila mtu amesikia ‘so’ siwezi kuzungumza lolote.”

cHanzo:GPL

No comments:

Post a Comment