Saturday 26 February 2011

HASHEEM THABEET AUZWA HOUSTON ROCKETS

Habari ambazo zimetufikia muda si mrefu uliopita zinapasha kwamba mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya NBA, Hasheem Thabeet (pichani) aliyekuwa akichezea timu ya Memphis Grizzlies, ameuzwa kwenda timu ya Houston Rockets ya jijini Houston, Texas katika mabadilishano maalumu baina ya timu hizo mbili.

Katika mabadilishano hayo, mchezaji Shane Battier aliyekuwa akichezea timu anayokwenda Hasheem (Houston Rockets) anajiunga na Memphis Grizzlies.

hasheem thabeet

Maendeleo ya Hasheem katika ligi hiyo ya NBA yamekuwa hayaridhishi. Ana kiwango cha vikapu 1.2 na rebound 1.7 kwa kila mchezo. Hicho ni kiwango cha chini sana kwa mchezaji ambaye alichaguliwa akiwa kama 2nd pick katika draft mwaka 2009. Aliyekuwa 1st pick katika mwaka huo ni Blake Griffin aliyekwenda Los Angeles Clippers.

Ni matumaini yetu kwamba kwa kwenda Houston mji ambao unaaminika kuwa na watanzania wengi zaidi nchini Marekani kuliko mahali pengine, Hasheem atajisikia kuwa “nyumbani” zaidi na atapata muda wa kucheza zaidi kitu ambacho anakihitaji sana ili kuendeleza mchezo wake ndani ya ligi hiyo yenye ushindani wa kila aina. Kila la kheri Hasheem.


sio mpenzi sana wa huu mchezo ila wajuzi mtuambie kama dalili hizi ni nzuri au mbaya kwa celebrity wetu huyu?

No comments:

Post a Comment