Friday 11 February 2011

KIBAKA ANAPOPATA KIBOKO YAKE

 

huyu kibaka inasemekana alimtaimu jamaa kwenye mataa akiwa na gari kwa kutaka kumuibia.
jamaa aliposhtuka na kumuona kibaka wake anateleza,jamaa akaona ngoja kaenda paki gari lake safi kamfuata kibaka.
kibaka alipoona jamaa anakuja kaokota mimawe jamaa kaendelea kumfuata si amtishie kisu!ndio kwaanza jamaa kazidisha munkari na kumkimbiza kumuwahi kisha kumnyanganya kisu na kuanza kumchoma nacho mwenyewe kibaka!.
eeh na yeye aonje kidogo makali ya kisu.isingekuwa wasamaria wema kumtoa kibaka hapa tungeongea mengine,hadithi hii inafanana na yangu siku moja nimetoka zangu kwenye mipakazo mitaa ya mw/nyamala narudi skani kuna kibaka alikua ananilia timing,mi niko mbele yeye nyuma yangu.

tatizo alikua anaongea sana nikamshtukia.basi nilipofika kona fulani namimi nikamsubiri safi kwa timing kali,nayeye anakuja na kisu basi ile anapinda kona alikutana na ngumi jiwe moja ya pua,kibaka sijui alidhani amedondokewa na tofali maana kwa mshtuko kisu kilimponyoka nayeye akadondoka chini kama mende,naenda kuokota kisu nigeuke loo kainuka hilo vumbi alilotimua alipoamka,wee acha maana nilibaki sina mbavu

No comments:

Post a Comment