Tuesday 8 February 2011

KHADIJA KIMOBITEL ARUDI TWANGA


MKURUGENZI wa kampuni ya African Stars Entertaiment (Aset), Asha Baraka,  leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mwanamuziki Khadija Mnoga (Kimobitel) ambaye ameamua kurejea katika bendi yake ya Twanga Pepeta.

Akizungumza katika ofisi za Aset zilizoko Kinondoni, jijini Dar es Salaam mara baada ya kumtambulisha msanii huyo aliyetokea bendi ya Extra Bongo, Baraka alisema kuwa Kimobitel ameamua kuejea katika bendi hiyo baada ya kuchoka na kile alichokiita “ubabaishaji” katika bendi hiyo ya awali iliyo chini ya mwanamuziki Ally Choki.

Nimeamua kurudi nyumbani kwani sikufukuzwa na mtu yeyote ndani ya Twanga Pepeta.  Niliamua tu kupumzika.  Mbaya zaidi, kule nilipotoka kumezidi sana tabia za ubabaishaji,” alisema Mnoga.

Wakati huohuo, Asha Baraka amewatambulisha waimbaji wengine kama Haji Ramadhani(bongo star seach) na Venance Joseph aliyetoka(bwagamoyo sound) na pia kumtambulisha  Martin Sospeter kuwa meneja mpya wa bendi hiyo baada ya kifo cha Abuu Semhando.

2 comments:

  1. yale yale......kesho ally choki.Mdau tumba

    ReplyDelete
  2. ha ha haaa,acha wewe kesho aly choki tena?sasa akiondoka yeye mchungaji kule wale kondoo wake waende wapi?ila wale watano walioenda kule nna mashaka hawatadumu,watarudi muda si mrefu twanga maana siwaamini kabisaaa

    ReplyDelete