Tuesday 8 February 2011

UKWELI WAJULIKANA SAKATA LA WATOTO 10 WALIOKUTWA SHIMONI


Sakata la watoto wachanga 10 waliofukuliwa na jeshi la polisi katika shimo moja maeneo ya Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wiki iliyopita limeingia katika sura mpya baada ya mama zao kujulikana.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Hospitali ya Mwananyamala  kunakotajwa kwamba ndiko maiti za watoto hao wachanga zilikotoka, umebaini kwamba wazazi wanaohusika na tukio hilo wanafahamika na wako katika makundi matatu.

MAKUNDI MATATU
Chanzo chetu cha habari ndani ya hospitali hiyo kimedai kuwa kundi la kwanza lililotajwa kuhusika ni machangudoa wanaopata mimba lakini hawako tayari kulea watoto, hivyo kufika hospitalini hapo kwa nia ya kutoa.

Imedaiwa kuwa machangudoa hao wanapofika hospitalini hapo huongea na baadhi ya wauguzi ambao baada ya kukubaliana kiasi cha fedha, huwawekea maji ya uchungu kisha kujifungua watoto wafu ambao hubaki hospitalini hapo kwa makubaliano kuwa watazikwa na watumishi kwa malipo maalumu.

Aidha, chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, zoezi la kutoa mimba hufanyika kwa siri. Imeelezwa kuwa  machangudoa hao wameshajenga  uhusiano mzuri na baadhi ya wauguzi ambapo wamekua wakiwapa fedha  kuanzia shilingi 30,000 na kuendelea ili kuharibu mimba bila uongozi wa juu wa hospitali kujua.


soma zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment