Friday 4 February 2011

WANAMUZIKI KIBAO WAHAMA TWANGA NA KUJIUNGA EXTRA BONGO


kichwa "FERGUSON"kimeanza
kichwa kingine rogert hega"caterpillah kimejiunga twanga pia


super nyamwela naye kaondoka

otillia boniface kulia nae kajiunga extra bongo
super danger (kijani)nae kachomokea twanga

alli choki akiwa na kikosi kizima kipya kilichojiunga naye

habari gonga link hii TWANGA PEPETA YAZIDI KUBOMOLEWA

hili nalo ni pigo jingine kubwa kwa ASHA BARAKA hasa baada ya wanamuziki wengine KHALID CHOKORAA na KALALA JR kuondoka na kujiunga na kundi lao MAPACHA WATATU.inaelekea asha hataki kukubali kwamba anawabana sana kimaslahi wanamuziki wake na kuwapendelea wengine,hii si mara ya kwanza kwa wanamuziki kumkimbia,inabidi akae na wanamuziki na kuwauliza tatizo hasa liko wapi,maana hii ni hatari na nadhani iko siku atakuja kushtukia bendi nzima imehama kwa mpigo kama ilivyotokea kwa koffi olomide.
hapa ukimuuliza maoni yake kuhusu hili jambo atakwambia "mi nimewasaidia sana hawa leo wamenifanyia hivi!mungu atanilipia".
hakuna swala la msaada wala kulipwa na mungu,hao wanamuziki wanafanya hiyo kama kazi na walipwe inavyotakiwa kadri ya kazi yao,sio kuwa-diktate tu kwamba mkiondoka twanga tu mtakiona,hii sio nzuri,dalili  kashaziona kwamba wanamuziki wake hawaridhishwi na mwenendo wa bendi.
inabidi arekebishe hilo haraka sana kabla bendi haijazimika ghafla na mashabiki kumkimbia,ASHA ametoka mbali na hii bendi na swala la kurekebisha ni dogo sana na naamini anaweza akiamua. 


2 comments:

  1. mzazi usiseme sana,mbona watarudi hao shamba la bibi,wanabadilisha hali ya hewa tu.Mdau tumba

    ReplyDelete
  2. teh teh ,najua kidau ya chief kiumbe ikiisha watarudi twanga

    ReplyDelete