Wednesday 20 October 2010

AJILIPUA NA PETROL BAADA YA KUNYIMWA KIBALI CHA UKIMBIZI SWEDEN NA KAFUNGWA MWAKA

maswala mengine utadhani utani,jamaa baada ya kuambiwa kwamba haitajiki hapa na anatakiwa aondoke haraka sana, akamwambia muelekezaji wake"subiri nakuja"kisha kaelekea chooni.kumbe alikua na chupa ya petrol kwenye mfuko wa jaket,kufika toilet jamaa kajimwagia petrol yake kichwani kisha kajipiga kiberiti,mara kafungua mlango ametoka anawaka kama mwenge wa uhuru vile.bahati nzuri wasamaria wakamuwahi na fire extinguisher haraka na wakafanikiwa kuzima moto na kumkimbiza hospital.na sasa waswede naona wameamua kama mbaya iwe mbaya tu maana jamaa alipotoka hospital badala ya kumgongea kama kawaida yao naona wamechange na kumzawadia jamaa kifungo cha mwaka mmoja jela.lakini jela ya hapa aah jamaa ni kama kaenda county hotel tu sio dili sana.na akitoka kama mungu wake mkubwa watampa.lakini kama ndo ana gundu ndio hivyo tena itakua alanda hiyoooo kisha kipawa ya kwao hiyoooo.
kweli watu wamepinda maisha haya.

No comments:

Post a Comment