Wednesday 20 October 2010

ALIKIBA ANYIMWA VIZA KWENDA MAREKANI


 ALI KIBA
Mwanamuziki wa Kizazi kipya Ali Kiba ambaye alikuwa aende nchini Marekani kwa maonesho kadhaa nchini humo amegonga mwamba mara baada ya ubalozi wa Marekani Kumnyima Viza ya kumruhusu kuingia nchini humo. Chanzo chetu cha habari kinasema Mwanamuziki huyo Mahiri ambaye anakubalika sana huko Ulaya na Marekani alifika Ubalozini hapo leo asubuhi kwa ajili ya kushughulikia Viza yake ili aweze kwenda nchini Marekani lakini aliambiwa na mmoja wa maafisa wa Ubalozi huo kuwa hawezi kupata Viza kwa sababu ya matatizo ya Pasipoti yake ya kusafiria. Hata hivyo inasadikika kwamba huenda mwanamuziki huyo alikuwa hajakagua pasipoti yake ambayo inaelekea imaisha hivyo alitakiwa kuomba nyingine kabla hajaenda kuomba Viza, lakini hakufanya hivyo! labda alikuwa hajui kama Pasipoti yake imeisha au huenda alikaidi kufuata utaratibu huo ambao umepelekea kumkwamisha katika safari yake hiyo. Ali Kiba ametoka Ubalozini hapo akiwa mwenye kunyong'onyea na kukata tamaa kwani haijajulikana kama angefanya onesho siku gani huko Marekani.

N:B.jamaa washaanza kubana maana hawatupendi kweli.

No comments:

Post a Comment