Tuesday 19 July 2011

NCHI IKO GIZANI,VIONGOZI HUSIKA WANAANDAA HONGO KWA WABUNGE KUPITISHA BAJETI!


Saa nyingine huwa nashindwa kuelewa kuwa tumelogwa na nani,katika miaka hamsini ya kujivunia uhuru badala ya kujivunia maendeleo ndio kwaanza tunazidi kuzama katika kina kirefu cha matatizo.hali hii inasababishwa na nini??
tusijifanye kama hatujui(RUSHWA)inazidi kulitumbukiza taifa katika matatizo makubwa,sasa imefika mahali rushwa inaonekana kitu cha kawaida kabisa,yaani hivi sasa mbongo ama mTZ akikuomba rushwa mahali popote pale ukashangaa shangaa atakuona sijui unatoka sayari gani,na nakuapia hutapata huduma yoyote ya muhimu unayohitaji mpaka utoe kitu kidogo,ukienda hospitali,polisi,uhamiaji,kila idara shughui ni hiyo,kichekesho sasa utaona matangazo makuuubwa ukutani"RUSHWA NI ADUI WA HAKI,USITOE WALA KUPOKEA RUSHWA"thubutu yako,jaribu kutotoa rushwa hospitali kama hujafa hapo na wao wanakuangalia tu,ama polis trafik kakukamata unaleta ubishi kutoa chochote gari lako utalisahau polis,na ukija kulipata tena utalia maana wamenyofoa vifaa kibao.hiyo ndio bongo

sasa tukirudi kwenye mada,jana tumeona maigizo mengine ndani ya bunge pale mbunge mmoja(nadhani hakuwemo kwenye mgao huyu) alipotoboa siri ya kiongozi wa wizara ya nishati na madini kuandika barua ya kutoa hongo ili bajeti yao ipitishwe bila kupingwa
baada ya hapo wabunge walikuja juu ile mbaya(si unajua kimesanuka)kutaka waziri na huyo kiongozi wajiuzuru.
kilichotokea waziri mkuu kaitia kwapani hiyo bajeti(badala ya kuwawajibisha waliohusika) ikaandaliwe upya(kukarabatiwa) na kurejeshwa tena baada ya wiki tatu.
sasa utaona jinsi hayo maigizo yanavyoendelea kwani viongozi wahusika wa hiyo kashfa hawatawajibishwa,na hiyo bajeti itarudi kama ilivyo labda itarekebishwa lugha tu,na ikirudi wabunge wataipitisha bila kupingwa.
then rushwa itaendelea kutolewa na wizara katika makampuni yanayohusika na kuzalisha umeme,na umeme hautakuwa unazalishwa inavyotakiwa na nchi itaendelea kukaa gizani mpaka hapo yesu atakaporudi.
hapa tunapoongea kuna makampuni makubwa makubwa ya kuzalisha umeme ambayo yapo kazini,na yanafanya kazi na yana watumishi kuanzia maofisa,wakurugenzi mpaka mafundi wapo.

 wanaenda kazini na ukiambiwa wanalipwa bei gani kwa siku utazimia,lakini bado giza linatoa muendelezo wa kuchapa bakora kila siku,ile kashfa ya dowans sijui iliishia wapi(sitashangaa kama washalipwa fidia yao kisha kupiga kimyaa)
watanzania tushasahau siku nyiiingi tuko busy kula kitimoto na bia
ninayo mengi ya kuongea lakini naona niishie hapo tu na kutoa shukrani kwa viongozi wa chama na serekali kwa kutufikisha hapa tulipo.

1 comment: