Thursday 7 July 2011

WASANII NA KUAZIMA SUTI ZA SHOOTING


msanii TINO anayeshutumiwa kuazima suti


suti iliyorudishwa nyalu nyalu




koti rangi yake suruali rangi yake

Habari zaidi gonga hapo chini


si mara ya kwanza wasanii kulalamikiwa kuhusu vitu wanavyoazima na kuvitumia vibaya,wadhamini wengi wanaowaazima vitu ikiwa ni pamoja na majumba,magari, vito vya dhahabu na vingine mwisho wanaishia kulalamika vitu vyao kutumiwa vibaya
na tatizo kubwa ni kwamba kila msanii ni director na pia kila movie wanazo-act tunaishia kuona magari na majumba ya thamani utazani tuko showroom ama real estate,na pia kuonyeshwa mapaja ya kina aunt ezekiel na irene uwoya mpaka tumechoka.
sio lazima muingie lawama kwaa ajili ya kuazima suti na magauni ili muonekane wa gharama wakati njaa kali.kila mtu anaijua hali halisi ya mtanzania na hasa nyinyi kuna haja gani ya kukimbilia kutuonyesha mko juu wakati tunaelewa kwamba hiyo ni show-off tu?
nilikua mstari wa mbele hapo nyuma kuweka movie zenu lakini baadae hata mimi zikanichosha maana hamna hadithi ingine ntaona zaidi ya mko chumbani kitandani,mapaja,ofisini,magari ya kina msofe na muzamill,nyumba za kina dotnata.
kwani hamuwezi ku-act vitu vingine katika mazingira ya kibongo bongo?wenzenu wanigeria ingawa wanatoa movie kila wiki lakini at least wana movie zingine ambazo utazipenda kwa mpangilio na kuonyesha mazingira halisi ya ki-afrika.
inabidi mbadilike jamani maana sasa watu wanachoshwa na hayo maigizo yenu,pia muwe wastaarabu mnapoenda kuazima vifaa kwa watu mu-act mpendeze sio mbaya lakini rudisheni mkimaliza shooting na muwe waangalifu msiviharibu mkapata lawama kama hizi.
ni hayo tu msinichukie kwa kutoa maoni yangu.  

3 comments:

  1. Yani Isack napenda kukusifu kwa matukio yako, hubabaishi habari,hutuwekei wauza sura,unatumia lugha vizuri iwe kingereza au kiswaili na km ni kuchangia unaweka point hasa. kuna viblog viwili 3 hapa sweden havina matukio ni kutuwekea wauza sura tu yani wazi kbs m2 hana cha kutuhabarisha watu ni wale wale habari hamna na km ipo basi kakopi toka kwenye blog nyingine.
    Yani blog sasa inakuwa km email address kila m2 anataka kuwa nayo mwishoe ni kuji9shushia heshima tu.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kbs hawana jipya hawa tena wanabowa mno sio kwamba hatuwapi sapoti tunawapa sn ila wanatuangusha. Wakifanya move yenye maisha halisi ya mtanzania inakuwa nzuri sn juu wanapatika kila ki2 nyumba,mavazi mpk madhari ila wakifanya za kishua ndo aibu km izo za kuharibu suti,kingereza cha ugoko, na kuonyeshana vichupi tu. yani ukishaangalia for 20 minutes walai u cn tel wats next mana zinafanana krb zote

    ReplyDelete
  3. hahahahhha@kaka Kitururu mbona waguna yakheee, ungekuwa bongo mbona ungewakoma maana hizi ndiyo zavi zako!!!

    ReplyDelete