Wednesday 27 July 2011

SAMAKI WENYE SUMU WAPATIKANA DAR

MAMA BLANDINA NYONI
 
Katibu Mkuu wa WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii
ndio aliyetoa hii habari peupe
 
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imetahadharisha kuhusu kusambazwa kwa zaidi ya kilo 1,000 za samaki wenye sumu sehemu mbalimbali za nchi na kuwataka wananchi washiriki msako iliouanzisha kuwatafuta.

Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa samaki hao ni sehemu ya kilo 124,992 zilizoingizwa nchini kutoka Japan.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tayari Serikali imeanza msako mkali kuwatafuta samaki hao, lakini ikaonyesha wasiwasi kwamba juhudi hizo huenda zisizae matunda kwa kuwa sehemu ya shehena hiyo imeshaingia sokoni.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Blandina Nyoni alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa samaki hao tayari wameingizwa katika masoko ya Dar es Salaam na Morogoro.

“Wananchi wanaombwa kutoa ushirikiano kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Idara za Afya za Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro na Jeshi la Polisi, ili samaki waliobaki wapatikane,” alisema Nyoni.

Nyoni aliutahadharisha umma kuwa athari za sumu inayohofiwa kuwapo kwenye samaki hao ni ya mionzi ya nyuklia ambayo kimsingi hujitokeza taratibu katika mwili wa binadamu.“Samaki wenye uzito wa tani 1.319 wanafuatiliwa na kumbukumbu zinaonesha kuwa wamesambazwa kupitia soko la Feri, Dar es Salaam, Morogoro Mjini na Kilombero,”alisema

Katika kuhaha ili kuokoa maisha ya Watanzania, Nyoni anasema: “Wizara inaviomba vyombo vya habari, viiarifu na kuielimisha jamii juu ya kuwepo kwa samaki hao wanaochunguzwa kwa kuhisiwa kuwa na madhara.”

Pamoja na juhudi hizo, alifafanua “kazi hii ya ufuatiliaji na uchunguzi, inaendelea usiku na mchana hadi samaki hao watakapopatikana.”
 
SAMAKI WAMEPATIKANA WAMEENDA KUTHIBITISHWA KAMA KWELI WANA MIONZI ARUSHAAAA!
 
bofya HAPA

No comments:

Post a Comment