Wednesday 13 July 2011

SHOW YA KIDUM UKUMBI UMEBADILISHWA SASA ATATUMBUIZA VÄSTBERGA ALLE 15-25




TAARIFA TULIZOLETEWA HIVI PUNDE NA DIRECTOR CLAY ONYANGO(ORKARINTE.SE)NI KWAMBA.

Kutokana na uwingi wa mashabiki wa msanii kidum,imeonekana kwamba ukumbi wa brommaplan utakuwa mdogo,hivyo waandaaji wamefanya jitihada za haraka kutafuta ukumbi utakaotosha mashabiki kwa wingi zaidi.
kutakuwa na nyamachoma ambayo itafanyika TANTO PARK HONSTUL ambapo mashabiki watapata fulsa ya kumuona msanii kidum kabla ya show
Nyamachoma itaanza saa tisa kamili (15-00) mchana na kuendelea mpaka mida ya watu kujimuvuzisha ukumbini,usafiri kwenda tanto park honstul ni kutumia tereni la kawaida mpaka honstul na utatokea mbele kushoto kisha nyosha moja kwa moja(kama hujawaona maganga wakielekea sehemu ya tukio)
RATIBA
nyama choma tanto park - 15:00
show ukumbini västberga alle 15-25 västberg  kuanzia saa 21:00-03:00 

kwenda ukumbini unashuka midsommarkransen,then tafuta midsommarvägen 10,fuata barabara kushoto ukipita chini ya daraja pembeni ya statoil petrol station dakika tano utaona mishumaa imewekwa kukuongoza ukumbini
unaweza book ticket yako kwa info@orkarinte.se au piga simu no 076 216 9132

ni mara ya kwanza kwa msanii kidum kuja sweden na jua limewaka hivyo ni kipindi muhimu kwa wapunguza steress kufanya kinachohitajika,unakula pamba na unyunyu,kisha unaenda tafuna nyamachoma kwa kwenda mbere huku ukijimiminia yale maji ya dhahabu inavyotakiwa baada ya hapo unaenda ukumbini kuserebuka na nyimbo za kidumu kama huna akili nzuri
mungu awape nini wana stockholmer zaidi ya hizi raha.
KARIBUNI 

No comments:

Post a Comment