Wednesday 11 July 2012

KOFFI OLOMIDE&QUARTER LATIN-DANGER DE MOT LIVE



marie paul(Wenge L Paris)


                                     Didier Masela
Adolphe Dominguez(Tata)




Alain Makaba(Prince)mpiga gita ambaye haijapata kutokea,hata ukimwamsha ndoto ya majinamizi usiku wa manane ukampa gitaa tu ni kama umempa mswaki.

Montana Kamenga


SOLEIR WANGA(kipenzi cha Koffi,soleir alikua mkali wa vokal quartier late nzima,hakuna cha fally wala ferre,lakini ndo hivyo kina fally walipotimua na yeye akafata mkondo kuanzisha bendi france kaangukia pua)
                                                                               Alain Mpela

BOURO MPELA

TUTU KALUDJI


Bill Clinton Kalondji(nafikiri mnamfahamu huyu jamaa katika mapinduzi ya bolingo Rap,kwa hint tu ni kwamba huyu mkali sauti yake ndio inaigizwa na KITOKOLOLO NA OBRIGADO wa wenge maison merre
Blaise Bulla
Kipindi hicho quartel latin ya ukweli,bendi ilitokea kujizolea sifa baada ya kuvunjika kwa wenge B.C.B.G,lakini kama ilivyo kawaida ya wacongo,kila mmoja anataka kuwa maarufu.

kuvaa gianni versace,dolce gabanna,gucci,sasa ndo inatokea mabendi yanaparaganyika kiajabu ajabu na wanamuziki wote wanaopaswa kuwa waitikiaji wanakimbilia kuanzisha bendi zao.sawa kuna waliofanikiwa kama Werrason,Fally Ipupa, Ferre Golla lakini wengi walichemka.
tukianza na musician wa kwanza kujitoa katika bendi na kuchemka ni kama mnamkumbuka Marie Paul,aliondoka kwa mara ya kwanza B.C.B.G na kwenda kuanzisha bendi yake Wenge EL Paris sababu ikielezwa kuwa alihisi kuna wanamuziki kwenye wenge B.C.B.G wanapewa upendeleo(alimaanisha J.B.Mpiana)sasa hivi imekuwa kawaida wanamuziki kuhama bendi na kuanzisha zao,hii hata bongo ipo,kina choki,banza, mapacha wawili,chalz baba.
ninasikitika siku zote nikiwaona wanamuziki waliokuwa wanatingisha kwa nyimbo zao kali leo hii hawasikiki tena,kuna Adolph Domingez,Alain Mpela,Bouro Mpela,Fille Nyaffu,Montana Kamenga,Soleir Wanga,Bill Clinton Kalondji,Tutu Kalodji,Emillia,Blaise bulla,Allain Makkaba.wote hawa na wengine wengi wala hawajulikani waliko,wengine wamejilipua mtoni.
wengine wamewekwa ndani na mijimama ili vile viuno wanakata kwenye steji wavikate kitandani(private show),wengine basi tu wamechooooka mbaya.
kuna siku hapa juzi nimemuona GODFATHER wa wenge B.C.B.G. enzi hizo DIDIER MASELA kwenye concert ya werrason kaitwa aungurumishe BASS GUITAR kama ilivyokuwa kawaida yake,hakufanya ajizi alilicharaza kweli ingawa ndo hivyo tena alikua yuko bwiiiii na alionekana kama vile Financial crisis ilikua inamtembelea mara kwa mara kumpa hi,sasa inasikitisha kwa wakongwe na mahiri wa muziki huo wa bolingo wakiwa wanaishia kwenda kunywa dengelua na kimpumu badala ya kuenziwa,shukrani zimwendee MZEE GURUMO maana yeye kakomaa na steji tu mpaka kieleweke,maaana ataacha ajira hiyo atakula wapi?tumemuona mzee Kipara akifa katika mazingira ya kimasikini kabisa,huku vijana aliowaingiza kwenye fani wakifa na kuzikwa kifahari na chama na serikali.sikuelewa hapo,katika sanaa nani alitumika zaidi kati ya mzee Kipara na Kanumba?nadhani tumeanza kumsikia mzee kipara zamani zaidi ya Kanumba,ingewezekana kabisa kwamba tungekuwa naye muda huu kama mzee huyu mkongwe wa sanaa angepewa msaada kama walivyopewa kina Kanumba na Sajuki.

lakini ndo vile mzee kajifia pale kigogo kwenye kijumba chake kinavuja na nadhani ni kwa kukosa matunzo mazuri na hakuna aliyejali.leo hii unashangaa kuona viongozi na misuti yao ya gharama na maconvoy ya migari lukuki inaenda kwenye msiba kisiasa kwa kubagua,
na nilikasirika kwa sababu msafara wao uliniweka road zidi ya masaa mawili,mbona kwa mzee kipara hawakuonekana?kina muhogo mchungu,mzee Jangala mjiandae vizuri maana nahisi mchango wenu bado hautambuliki katika sanaa kama mwenzenu mzee Kipara.
inasikitisha sana

No comments:

Post a Comment