Na Shakoor Jongo
KATIKA kukamilisha mfungo wake
wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’
amekubali kupatanishwa na mama yake mzazi, Miriam Sepetu, hivyo
kukamilisha usemi kuwa mtoto hakui kwa mzazi wake, Ijumaa limeshiba.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Wema, baada ya staa huyo
kutofautiana na mama yake kisa kikiwa ni mahojiano aliyofanya mzazi huyo
runingani ambayo hayakumpendeza Wema, hivi karibuni wamekutanishwa na
kurejesha amani iliyokuwa imetoweka kati yao.
“Mimi najua undani wa
ishu nzima, tangu yale mahojiano na nyiye (Global) mkaandika kuwa mama
Wema alimtia aibu mwanaye, hali ilikuwa mbaya hadi juzi walipopatanishwa
ndiyo wamerudisha ushosti wao,” kilisema chanzo hicho.
WAZEE WAWAPATANISHA
Chanzo chetu kilidadavua kuwa pamoja na Wema
kwenda kumwangukia mama’ke, kuna wazee ambao walitinga nyumbani kwa
Wema, Kijitonyama ‘Hollywood’, Dar waliotoka upande wa mzazi huyo ambao
walikwenda kumsihi afanye hivyo.
“Hazikuwa jitihada zake peke yake
za kutaka kumaliza tofauti kati yake na mama’ke bali wale wazee takriban
wanne walizungumza na Wema na kumwelekeza namna ya kumaliza tofauti
zake na mzaa chema huyo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Hao
wazee ndiyo waliwakutanisha kwa mama Wema, Sinza-Mori, Dar na kumaliza
chokochoko zote na sasa Wema na mama’ke mambo ni ‘mswaano’.
HALI ILIKUWA MBAYA SANA
Chanzo hicho kiliendelea kushusha data
kuwa kulikuwa na ulazima wa Wema kutinga kwa mama’ke na kumwangukia
kwani suala hilo lilikuwa likimpasua kichwa na kusababisha hali kuwa
mbaya kati ya wawili hao kwa sababu hakukuwa hata na salamu.
WEMA ASHINDA KWA MAMA’KE
Baada ya kusikiliza maelezo hayo kutoka
kwa chanzo, Julai 23, mwaka huu saa 5 na sekunde 35 asubuhi, Ijumaa
lilizungumza na Wema kutaka kujua alikuwa wapi wakati huo ambapo alijibu
kuwa anaenda kwa dada yake kumchukua mtoto aliyemtaja kwa jina la Sasha
kisha kwenda kushinda naye Sinza-Mori kwa mama yake.
Alipoulizwa
kama ni kweli kuna wazee walimfuata na kumpatanisha na mama yake, staa
huyo wa muvi ya Super Star itakayoingia sokoni Agosti alikiri kutokea
kwa suala hilo.
HUKO NYUMA
Wiki kadhaa zilizopita, Wema na mama yake walitibuana
baada ya mzazi huyo kuwatemea mbovu mashosti wa mwigizaji huyo alipokuwa
akihojiwa runingani.
chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment