Monday, 23 July 2012

MDAU AGREY URIO AFANYA BBQ PARTY YA KUFAMTU U.K.


Aggrey akikagua kama nyama ziko tayari.
Mr & Mrs Aggrey Urio katika pozi.
Mwenyekiti wa Tanz- UK, Dk Lusingu akifurahia jambo pamoja na Masija na Sheilamina.
Mdau akileta mkaa kuendeleza makamuzi ya kuchoma nyama.
Nyama zilichomwa zikachomeka.
Muda wa msosi ulipowadia.
Mr & Mrs Aggrey Urio wakila pozi na wadau.
---
Salaam,
Siku ya Jumamosi tarehe 21.7.12 mdau Aggrey Urio alifanya sherehe ya kuchoma nyama hapa mjini Reading kusheherekea siku yake ya kuzaliwa ikienda sambamba na kuwatambulisha wadau mke wake  Eunice aliyekuja rasmi kutoka Tanzania. Aidha Aggrey alichukua fursa hiyo kuwashukuru wadau wote waliomwezesha kufanikisha kufunga ndoa yake nyumbani Tanzania hivi karibuni.
Mmojawapo wa wageni waalikwa alikuwa Mwenyekiti wa TANZ- UK, Dk John Lusingu.
Asanteni,
Urban Pulse Creative

No comments:

Post a Comment