Thursday 26 July 2012

Waasi wa M23 washambuliwa zaidi Goma



Helikopta za majeshi ya Umoja wa Mataifa yameshambulia maeneo ya waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Ripoti zinasema kuwa mapigano makali yanaendelea kilomita 50, kaskazini mwa moji wa Goma.
Watu wanaotoroka makaazi hao wamewaambia BBC kuwa wanajeshi wa serikali wamekuwa wakitoroka vita.
Vita hivi vya sasa vilianza tangu mwezi wa April ambapo Umoja wa Mataifa nad Congo zikilaumu Rwanda kuwa kusaidia waasi.
Hata hivyo Rwanda imekanusha madai hayo.
Kufuatia mapigano hayo watu zaidi ya 200,000 wametoroka makaazi yao .
Wiki iliyopita waasi wa vuguvugu la M23, ambao Umoja wa mataifa unasema wanafadhiliwa na Rwanda, walitisha kuuteka mjini wa Goma, ambao ni kituo muhimu cha jeshi la kitaifa.
Kwa wakati huu mapigano bado yanaendelea umbali wa kilomita hamsini kaskazini mwa Goma katika eneo la Rutshuru.
Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema raia wengi wamehama makwao na kukimbilia mjini Goma na kutafuta afueni katika kambi za Umoja wa mataifa katika eneo hilo.

BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment