Na Waandishi Wetu
Mwanamitindo Jacqueline Patrick ambaye pia ni Miss Ilala no.3, 2005
anadaiwa kumtelekeza mumewe Abdullatif Fundikira aliyepo mahabusu katika
Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam kwa madai ya kujihusisha na
biashara haramu ya madawa ya kulevya.
Akizungumza na Amani, rafiki wa
karibu na mwanamitindo huyo alisema kuwa wenzake wanamshangaa Jack kwa
kitendo cha kumtosa mumewe wakati anafahamu yupo katika matatizo
makubwa.
“Kiukweli anachofanya Jack si uungwana kabisa, we fikiria
tangu mumewe akamatwe (Mei mwaka huu), hajawahi kwenda mahabusu
kumtembelea au hata siku ya mahakamani kuhudhuria kusikiliza kesi yake
inavyoendelea, yeye na starehe, starehe na yeye,” alisema shostito huyo
akiomba kuhifadhiwa kwa jina lake.
Akiendelea kuzungumza, rafiki huyo
alisema kuwa kitu kingine ambacho anaamini kuwa ndoa ya Jack ni ndoano
ni kitendo cha kuondoka nyumbani kwake na kutimkia nje ya nchi bila
mumewe kuwa na taarifa.
“Yaani huyu mwanamke ni wa ajabu sana, hivi
ninavyokwambia yupo nje ya nchi huku mumewe akiwa anateseka mahabusu,
mbaya zaidi mume hajui,” alisema.
Baada ya kusikia kauli hiyo, Amani
lilianza kumsaka Jack kupitia simu yake ya mkononi ambapo muda wote
ilionekana haipo hewani lakini kupitia udodosi wa paparazi wetu,
lilimnasa staa huyo juu kwa juu kupitia mtandao wa What’s Up ambapo
mahojiano yalikuwa hivi:
Shakoor: Jack ningependa kufahamu upo wapi kwa sasa maana nakutafuta kwenye simu yako ya mkononi sikupati?
Jack: Shida yako nini? Sihitaji stori wala promo ya aina yoyote kutoka kwenu.
Shakoor: Mbona umefika mbali? Hata ninachotaka kukwambia hujakisikia unaanza kuwa mkali.
Jack: Hapa hatuchezi drama hicho ndicho ninachoongea, nipo bize na mambo yangu, naomba niache.
Hata
hivyo, Jumatatu iliyopita, paparazi wetu mmoja alifunga safari hadi
nyumbani kwa nyota huyo, Mbezi, Dar es Salaam ambapo watu waliokutwa
ndani walisema Jack amesafiri kwenda ughaibuni bila kutaja jina la nchi
aliyoenda.
Mtu wa karibu na Jack alipopatikana na kuulizwa alipo
mwanandoa huyo, aliweka wazi kuwa yupo nchini Finland lakini hakusema
amefuata nini huko.
“Mimi ninavyojua Jack yuko Finland, sasa lini atarudi au amefuata nini huko, sijui,” alisema.
No comments:
Post a Comment