Friday 6 July 2012

PEDESHEE NDAMA AHUSISHWA KISANGA GARI LA WOLPER


Gari la Wolper aina ya BMW X6.
Jacqueline Masawe ‘Wolper’.
               NDAMA MUTOTO YA NGOMBE AKIZIMWAGA HUKU BAADA YA KUZIPIGA KULE
Na Gladness Mallya
SAKATA la kukamatwa kwa lile gari la kifahari aina ya BMW X6 lenye thamani ya takriban Sh. milioni 175 la staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe limeibua kisanga kipya, Ijumaa lina kila kitu mkononi.HABARI BILA WASIWASI
Habari bila wasiwasi zimeeleza kuwa pedeshee maarufu jijini Dar es Salaam, Mohamed Ndama a.k.a Ndama Mtoto wa Ng’ombe ndiye aliyemwingiza Wolper mkenge hivyo jamaa huyo ametiwa mbaroni akidaiwa kuhusika kuliingiza Bongo kinyemela.
Kwa mujibu wa chanzo kisichokoroma ambacho ni rafiki mkubwa wa Wolper, Ndama aliwekwa nyuma ya nondo katika Kituo cha Kati (Central), Dar Jumanne wiki hii baada kutajwa kuwa alihusika na uingizaji wa gari hilo hapa nchini.
Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa mchumba wa Wolper, Abdalla Mtoro ‘Dallas’ au Rais wa Ununio alitoa fedha kwa pedeshee huyo na kumtaka atafute gari la kifahari kwa ajili ya mchumba’ke (Wolper).
GARI LENYE HADHI YA WOLPER
Kilidai kuwa katika kutafuta gari lenye hadhi ya Wolper ndipo akampatia mwigizaji huyo lile BMW X6 na kubandikwa namba za usajili T 574 BXF.
TURUDI NYUMA KIDOGO
Katika habari ya kukamatwa kwa gari hilo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, ilielezwa kuwa lilikamatwa kwa sababu liliingizwa nchini bila vibali husika na pia kudaiwa ushuru unaokadiriwa kufikia Sh. milioni 70.
TUENDELEE NA CHANZO
“Unajua Ndama aliwapiga changa la macho Wolper na Dallas kwa sababu alipewa madaraka yote ya kutafuta gari hilo la kifahari.
“Ilikuwa ni vigumu kwa Wolper kutia shaka kwa sababu alipokabidhiwa lilikuwa na ‘dokumenti’ zote na ndiyo maana akawa anatanua nalo bila wasiwasi, lakini ndo hivyo ngoja tuone itakuwaje,” kilisema chanzo chetu cha kuaminika na kuongeza:
“Jumanne ndiyo aliitwa Central akahojiwa kwa saa kadhaa na Wolper akiwepo.
“Baada ya mahojiano pale kituoni hadi jioni ndipo akatupwa ‘lokapu’.
“Sijui kama alitoka kwa dhamana au alilala pale kituoni, fuatilieni.”
Baada ya kumwagiwa data, Ijumaa liliingia mzigoni ndipo likafanikiwa kupata ukweli kuwa Ndama alifunguliwa jalada la kesi namba CD/RB/7005/2012 na CD/IR/2624/2012.
KOVA ANASEMAJE?
Jumatano wiki hii, Ijumaa lilifunga safari hadi ofisini kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ili kulizungumzia tukio hilo lakini jitihada ziligonga mwamba baada ya kumsubiri muda mrefu kwa maelezo kwamba alikuwa kwenye kikao nyeti.
WOLPER ANAKATAKATA
Alipotafutwa Wolper alikuwa akikatakata simu kila alipopigiwa kwenye kilongalonga chake cha kiganjani.
TUMEFIKAJE HAPA?
Gari la Wolper lilikamatwa Juni 28, mwaka huu na kampuni ya Mnada ya Majembe kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuingizwa nchini kinyemela na kutolipiwa ushuru kwa muda wa miaka 5.
NINI HATIMA YA GARI HILO?
Inavyoonekana jeshi la polisi linakamilisha uchunguzi wake hivyo hatima ya gari la Wolper itajulikana hivi karibuni ambapo lazima litaondoka na mtu, soma magazeti ya Global Publishers.

CHANZO:GPL

NB:HUYU PEDESHEE NDAMA SI ALIWAHI KAMATWA KWA KUHUSISHWA NA KUUZA VIUNGO VYA ALBINO?ILE KESI SIJUI ILIISHIA WAPI MAANA JAMAA BADO ANAENDELEA TU KUWALIZA MITAANI,KWELI BONGO BONGOLALA

No comments:

Post a Comment