Monday, 2 July 2012

WABUNGE WAKIELEKEA BUNGENI,ZAMANI NA SASA

E
hii ndivyo ilivyo,kwa sasa viongozi wetu walivyo wabinafsi wanajinunulia wao tu ma VX V8 yakutosha kuji enjoy maisha wakati raia wanakufa kwa kukosa huduma mahospitalini na ugumu wa maisha,inasemekana hilo gari moja la kifahari bei yake ni sawa na kununua mashine moja ya CT SCAN
.juzi hapa nimesikitika kuona habari mwananchi mmoja kavunjika mguu huko tanga na kufikishwa hospitali ya wilaya hakuna mashine ya X RAY.!viongozi hawa hawaoni aibu?
nani anayejali,hawa wenzetu wabunge ndio waliopewa dhamana ya kutunga sheria lakini badala yake wamegeuka kutunga sheria za kuneemesha matumbo yao.ila kwa sasa ni swala la muda tu wananchi wataghairi,maana kumekuwa na gap kubwa kati ya wanasiasa na wananchi.mwanasiasa sasa hivi ni mtu mkubwa kiuwezo kwa sababu hayuko pale kwa jili ya kutetea maslahi ya wananchi,bali kutetea maslahi ya tumbo lake na wanae.mageuzi yatakuja Tanzania maana adui yako mwombee njaa,na kwa sasa raia wana njaa kwel kwel,huku viongozi wakipiga usingizi kwa kushiba na kuvimbiwa.

No comments:

Post a Comment