Tausi Ally
MAHAKAMA ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya Euro 2 milioni, sawa na Sh3.1bilion inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania, nchini Italia, Profesa Costa Mahalu na Ofisa Utawala wa ubalozi huo, Grace Martin.
Hukumu ya kesi hiyo iliyokuwa ikinguruma mahakamani hapo kwa miaka kadhaa sasa, itasomwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mgeta.
Profesa Mahalu na Grace wanakabiliwa na mashtaka sita likiwemo la uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara hiyo.
Mei 8 mwaka huu Grace ambaye alikuwa Ofisa wa Utawala aliieleza mahakama hiyo ya Kisutu kuwa Balozi Mahalu hakuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha, bali alileta faida kwa taifa kwa kuwa na jengo zuri na kwamba anahitaji kupewa shukrani.
Akiongozwa na Wakili Mabere Marando kujitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili, Grace alidai kuwa kwa ufahamu wake Balozi Mahalu hakuisababishia serikali hasara kwa kuwa manunuzi yalileta faida na nchi kupata jengo zuri na hakuna fedha zilizopotea.
“Mheshimiwa kwa ufahamu wangu, Balozi Mahalu mashtaka yote sita yanayomkabili hakuyatenda, aliwasilisha mikataba miwili kama taarifa iliyofanyika kihalali,”alidai Grace.
Aliendelea kuiomba mahakama itupilie mbali tuhuma hizo na kwamba madai ya kuwa Balozi Mahalu alitumia risiti ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia kuidanganya serikali kuwa mwenye nyumba amelipwa fedha siyo ya kweli.
Hata hivyo, akiongozwa na Wakili Marando, Grace alihoji ni kwanini upande wa Jamhuri haukumleta mmiliki wa jengo hilo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia kukana risiti hiyo au Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( Takukuru), Edward Hossea na Fungo kuulizwa juu ya ununuzi wa jengo hilo kwa sababu walikwenda nchini humo kufanya uchunguzi.

No comments:
Post a Comment