Thursday 18 November 2010

AJALI AJALIII KENYA



kuna kipindi nilikuwa nakaa mbeya miaka fulani,kwenye kamji wanaita nzovwe.ni pembeni ya main road ya kwenda zambia,hapo pahala palikuwa panasifika sana kwa magari kupiga sarakasi kama hizi.mpaka tukawa tumezoea udogoni enzi hizo ikawa ni kama unaangalia game kumbe watu wanakufa masikini.katika ajali hizo kwakweli niliona ajali za kila aina pale na pia nishaona majeruhi wa kila dizaini maana hata dokta wa I.C.U. hanifikii.nishaona mtu kapasuka fuvu la kichwa damu inachuruzika kama bomba,pia siku pick up moja ilianguka pale tukashuhudia mtu utumbo ukiwa nje kabisa,kitendo cha kuona watu wamevunjika miguu ama kukatika mikono ilikuwa kawaida kabisa,ni sehemu hiyo hiyo pia mi mwenyewe nishawahi kugongwa vibaya sana na peugeot 405 enzi hizo nikavunjika mguu lakini waliunyoosha,shukrani madokta enzi hizo maana ingekuwa sasa sijui ingekuwaje,pia kuna siku nimeshuhudia gari ikiacha njia nilikuwa na mdogo wangu imma siku hiyo ingempata angekufa,maana iliacha njia kwa spidi ya ajabu na ikawa inakuja upande wake lakini mungu saidia kulikuwa na nguzo ya bomba la maji  mbele.mdogo wangu alikuwa kasimama tu kaduwaa anaiangalia hiyo gari mwee. ile gari ikaishia kugonga ile nguzo tukashuhudia waliokuwa abiria wakichomoza kwenye kioo cha mbele kilichopasuka damu chapa chapa,kwa woga sie tukatoka baruti vibaya sana.hizi story ni za ukweli kabisa wandugu si za kutunga.

No comments:

Post a Comment