Tuesday 9 November 2010

SNOW INAANGUKA MDA HUU HAPA STOCKHOLM



hali ya hewa leo,hizi picha nimepiga mda huu huu

leo toka asubuhi mda wa kwenda mihangaikoni kulikuwa na kiubaridi na upepo wa ajabu,na kuanzia mida ya saa nne kukawa na kimvua cha hapa na pale then snow nayo ikaanza kuanguka.mpaka muda huu inaendelea na wataalam wanasema itafikia kiasi cha decimeter 2.haya shughuli ndio imeanza maana ukifika muda kama huu hawa wenzetu huko majiani wanakua wamenuna hao,hamna cha salamu wala kuchekeana ni bati bati tu he he he,lakini summer aaah mchekea.ndio kipindi kimefika cha mtu kujipigilia makoti,masweta na majacket na buti za kufa mtu,mkipima uzito baada ya kuvaa ki winter-winter msije kujisahau mkadhani labda mmenenepeana ma-afya ya nguvu,inabidi urudie tena kujipima uzito ukiwa bafuni kwako bila miguo then ndo utajua ni kilo ngapi huwa unajitwika baada ya kutundika mabuti,masweta,majinsi,mitandio makofia,maglovus.kama hujajikuta kila siku unajitwika mizigo ya kilo kama 30 kwenda kazini na kurudi.tahadhari sijakwambia usivae.

No comments:

Post a Comment