Monday 29 November 2010

FILAMU YA OFF SIDE KUZINDULIWA KINSHASA

Filamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kuingia katika soko la filamu Tanzania, ikiwa inaigizwa na wasanii mashuhuri wa hapa nchini Steven Kanumba, Vicent Kigosi na Irene Uwoya itazinduliwa kwa mara ya kwanza Congo.

Ikiwa inasambazwa na Steps Entertainment, hii inaonekana kwamba wasamabzaji hawa wanajribu kupanua soko kwa kuweza kushirikisha wadau wengi katika filamu. Kuvuka mipaka ni hatua kubwa katika Tasnia ya filamu Tanzania.
Steven, Vicent na Irene wataelekea huko wakiambatana na wasamabzaji wao na utafinyika uzinduzi mkubwa na wa mara ya kwanza kutokea katika Tasnia ya filamu Tanzania. Steven na Vicent wanaandika historia Tena
Congo kaeni mkao wa kula, Filamu hilo linakuja
chanzo:hapa


sijui imekuwaje kuwa na idea ya kuzindua movie ya kiswahili congo D.R.C,lakini yote ni ubunifu tu na vijimambo sie tunasubiri tu hilo muvi mitaani

No comments:

Post a Comment