Saturday 13 November 2010

NDOA YAINGIA SHUBIRI


waliokuwa maharusi
Ndoa iliyokuwa ifungwe kati ya Bwanaharusi, Joseph Kibarabara na mkewe mtarajiwa, Warda Halfa, imetibuka kufuatia Bibiharusi huyo ‘kutekwa’ na kufungiwa chumbani na mwanaume anayedaiwa ni hawara yake wa zamani, Risasi Jumamosi linamwaga mambo hadharani.

Varangati hilo lilijiri Novemba 7, mwaka huu maeneo ya Ukonga, Dar baada ya aliyekuwa Bibiharusi mtarajiwa, Warda kuacha njia ya kuelekea kanisani kufanya mazoezi ya kufunga ndoa ‘riheso’ na mumewe mtarajiwa, Kibarabara na kumfuata mwanaume aliyedaiwa ni hawara yake aitwaye John Laurent.
MCHEZO ULIVYOANZA:
Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika, hawara huyo alimpigia simu Warda siku moja kabla ya ndoa na kumuuliza kama habari anazozisikia anaolewa ni za kweli.
“Laurent alimpigia simu Warda kumuuliza kama kweli anaolewa, akamjibu ndiyo, akamwomba aende nyumbani kwake ‘wakachakachue’ kwa mara ya mwisho, naye akakubali akaenda,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliendelea kuweka wazi kwamba, wakati Warda anakwenda kwa mwanaume huyo, mumewe Kibarabara alishampigia simu akimtaka wakutane kanisani kwa ajili ya ‘riheso’, wito ambao mwanamke huyo aliupuuza
Habari zinadai, baada ya Warda kufika kwa ‘jamaa’ yake wa zamani walichakachua kweli, lakini ghafla mwanaume huyo alimnyang’anya simu kisha akaizima na kutoa funguo kwenye kitasa cha mlango huku akimwambia ‘HAKUNA KUTOKA’ licha ya kwamba alikuwa akijua mwanamke huyo atafunga ndoa kesho yake saa tisa Alasiri.


Ikazidi kuelezwa na chanzo chetu kwamba, njemba huyo aliendelea kustarehe na mke mtarajiwa wa mwenzake hadi Jumapili saa kumi na moja Jioni alipomwachia wakati ndoa ilikuwa ifungwe saa 9 Alasiri katika Kanisa la Sabato Ukonga (SDA).

MBINU ZA KUUA SOO ZAFANYWA:
Baada ya kubaini kosa kubwa walilolifanya, hawara huyo alimchukua Warda hadi kwenye Zahanati moja maeneo ya Manzese, Dar na kudanganya kwa daktari kuwa, mwanamke huyo alianguka ghafla na kupoteza fahamu maeneo ya hayo hivyo kupatiwa matibabu ya dharura.
Baada ya hapo, Warda alirudi nyumbani kwao ambako alikuta ndugu, jamaa na marafiki wamevimba sura kwa hasira, wengine wakikaribia kutumbuka kama siyo kupasuka.

Wakati hayo yote yanafanyika, inasemekana Bwanaharusi ambaye tayari na ‘bestman’ wake walikuwa ndani ya suti mpya, alikuwa akiwakaba koo wazazi aliowalipa mahari akidai chake huku habari nyingine zikinyetisha kuwa, alishabonyezwa na wadaku kuhusu mchezo mzima wa Bibiharusi na jamaa yake wa zamani.

KAMATI KUU YA FAMILIA YAKETI KWA DHARURA:
Kufuatia tukio hilo la aibu chanzo kinadai, ndugu wa pande zote mbili waliketi kwa dharura nyumbani kwa shangazi wa Bibiharusi, Kimara Baruti, Dar ili kutafuta mwafaka na ndipo ghafla alitokea Warda akiwa amechoka ile mbaya

Ndipo alipobanwa kisawasawa aeleze kinagaubaga nini kilitokea hadi

akaitumbukiza familia yake katika aibu kama ile, lakini wakati akimeza mate ili kujieleza, liliibuka varangati zito lililosababisha Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Magomeni ‘Mviringo’, Mokola Maulid aliyekuwa kwenye kikao hicho kama ndugu, kupigwa baada ya upande wa Bwanaharusi kupandwa na jazba.

Kufuatia tafrani hiyo kuchukua muda mrefu huku wanandugu wa pande zote wakiwa na hasira, hasa mawifi, watu wenye hekima walishauri kwenda Polisi Kituo cha Mbezi Luisi, Dar ambako ukweli utabainika.

Safari ilianza mpaka Kituo cha polisi na kupokelewa na maafande wenye sifa zote katika mambo ya sheria na ulinzi wa raia huku wakiweka sawa kitabu kikubwa cha ‘kaunta’ kwa ajili ya kuchukua maelezo ya pande zote mbili.
BIBIHARUSI NA AFANDE MASAITOO:
Akielezea mkasa huo mbele ya Sajenti Masaitoo wa kituo hicho cha Polisi, Biharusi ambaye sherehe ya kumuaga ‘Send Off’ ilikuwa ya kukata na shoka ilifanyika Alhamisi ya Novemba 4, 2010, alisema:

“Jamani nisameheni ibilisi alinipitia. Jana nikiwa Manzese, mwenzangu (Kibarabara) alinipigia simu akitaka aniletee gari la kunipeleka kwenye ‘riheso’ lakini simu yake ilipokatika, hawara wangu wa zamani, Laurent naye alinipigia simu, akinitaka niende nyumbani kwake Kinondoni ‘tukaagane’.

“Nilipofika tuliagana, lakini baada ya kumaliza shida zake nilimwambia aniache niwahi kanisani kufanya riheso, yeye akagoma akaniambia hakuna kwenda popote na kunifungia mlango kwa

Afande Masaitoo alipomuuliza kwanini hakupiga kelele kuomba msaada kama na yeye hakunogewa na uhondo, Bibiharusi Warda aliinamisha kichwa huku akisema: “Ibilisi alinipitia.”
Afande Masaitoo alimuuliza tena: “Kama mchumba ‘ako alikupigia simu akuletee gari kukupeleka kwenye riheso kanisani, kwanini uliacha safari hiyo na kwenda nyumbani kwa hawara?”

Biharusi: “Nilijua nisingechukua muda mrefu na ningeweza kuwahi kanisani baada ya kumalizana na mpenzi wangu wa zamani.”
BWANAHARUSI AKATAA KUFA NA TAI SHINGONI:

Baada ya Bibiharusi huyo kuweka hadharani ‘mauchafu’ yake hayo, Afande Masaitoo aliyekuwa akiongoza kikao cha usuluhishi alimshauri Bwanaharusi mtarajiwa kumsamehe mchumba wake na kuendelea naye (afe na tai shingoni), vinginevyo aende mahakamani kufungua kesi ya madai.

Bwanaharusi alifyatuka pale pale mbele ya umati kuwa, hawezi kumoa tena mwanamke huyo aliyethubutu kwenda ‘kuchakachua’ siku moja kabla ya ndoa kwani amemdhalilisha kwa kiasi kikubwa.
Habari za ndani zinadai kuwa, bajeti ya ndoa hiyo ikiwa ni pamoja na sherehe za harusi iligonga shilingi milioni kumi na mbili, tayari Ukumbi wa Holland uliopo Msimbazi Centre jijini Dar ulishalipiwa shilingi laki nane huku sare za harusi zikigharimu milioni kadhaa, vinywaji na chakula vya kumwaga, ndugu wengine wakitoka nje ya Dar kuja kuserebuka.

source:GPL

DAH JAMAA ALIINGIA KINGI VIBAYA SANA KUOA HIKI KIMEO,ASHUKURU MUNGU KAMUONYESHA MAPEMA KAMA HUYO SI MKE DUH.

No comments:

Post a Comment