Wednesday 3 November 2010

MONA SAHLIN KUCHUNGUZWA NA KITENGO CHA RUSHWA BAADA YA KUKUBALI TICKET YA BURE GOLF


Mwanamama nae huwa hakomi maana wanamuandama kweli na vi-kashfa vidogo dogo.haya baada ya ile ya kununua chocolate kwa kadi ya benki ya serikali sasa imekuja nyingine kwamba kwanini alikubali kupokea ticket ya complimentary kuingia bure kwenye mashindano ya golf!hii ndio raha ya nchi zilizoendelea maana kila kitu wewe kama kiongozi lazima uwe responsible hawakuachi,natamani sana sheria kama hizi zingetumika bongo ipasavyo.maana viongozi wetu kule kwanza sio mpaka wapewe wenyewe wanaomba rushwa live,na ole wako uwanyime.hii mambo ya kutokulipa viingilio ndio kabisa.tena kama wewe ndio unakatisha ticket ole wako umdai kiingilio sehemu yoyote utasikia "unanijua mimi,unanidai kiingilio"na hapo ataanza kukutishia maisha na kibarua chako vilevile.

ukitaka kuisoma hiyo habari na kufanya zoezi la kutema yai bonyee HAPA

No comments:

Post a Comment