Tuesday 23 November 2010

SHANGWE ZA STOCKHOLM SODRA IJUMAA

baada ya kutoka movie mimi na mamaa bella XXL,tukaona muda bado unaruhusu yanini kurudi nyumbani kwenda kugombania remote,tukaona twende sodra tukalicheze sendemaa ya moto.na yeye sababu ni mpenzi wa sendema hakujivunga.

mlangoni nikakutana na jamaa yangu huyu bwana nsunsulima maganga mwelee mwelee aliponiona akacheeeeeeka
 .
kuzama ndani nikamkuta pia tamim a.k.a ngumi tofali

mkuu huyu ni mtaalamu wa kutandika zile za kina mike tyson na muhamad alli lakini hapa imebidi atundike daluga kwanza hadi hapo baadaye
tukafurahi kuonana maana tulipoteana toka siku moja kuonana kwenye kazi moja ya ku-lift vitu vizito sana,mi nilichemka maana weight yangu na hiyo kazi vilikua haviendani,na ukizingatia jana yake nilikua nimeweka vyombo,basi weee,lakini mshkaji aliokoa jahazi.

bwana lomu masai nae alikuwepo,naona alikuwa tayari sailensa

nikakutana pia na ndugu zangu hawa,huwa tunaonana sana mitaa ya kati pale kwa yesu kuna raha


nikakutana na mkuu huyu pia tulifurahi kufahamiana zaidi.

ilikuwa safi sana maana unajua tena hapa kila siku mtu unaishia kupiga makoti makoti,kisha treni nenda rudi,kisha nyumbani ule ugali na vibawa ulale miaka nendaa rudii,inakuwa njema sana unapoenda mahali uankutana na wamatumbi wenzio mnabonga kiswazi huku story na report za hapa na pale,sio kila siku tuna addopt tabia za kununaa tuu ndani ya matreni na mabasi kama wenzetu hawa,mwisho tunaishia kunuka midomo.

No comments:

Post a Comment