Friday 26 November 2010

BAADA YA KUTUHUMIWA KUTAPELI MIL8 MENEJA MUJIBU WA FM APIGWA CHINI

meneja wa fm academia"NGWASUMA" mujibu hamis
habari zaidi zifuate chini hapo
jamaa katoka mbali sana na hii bendi.nakumbuka kipindi fm wamefungwa huyu mujibu ndio alikuwa mshabiki wa bendi hiyo tu na kipindi chote bendi hiyo walipowekwa ndani ni mujibu ndie aliyekuwa anawapelekea msosi.mpishi akiwa loving chitoto(sijui naye kapotelea wapi).baada ya hao fm kutoka jela wakafurahi sana na roho ya huyu bwana mujibu kuwasaidia na ndio wakamtunuku kumpa cheo hicho asimamie bendi.nakumbuka fm walipotoka jela walikuwa hawana kitu kabisa na wanakaa gesti moja pale kinondoni jirani na chez ntemba.wakajitahidi kujichangisha kidogo nakumbuka walinunua drum na gitaa "vyote mchina"wakaazimaazima na amplifier na baadhi ya vyombo.well nakumbuka vizuri nilikuwa kameneja pale club arcade kipindi hicho na nilishawishi uongozi wawape tenda wapige muziki pale baada ya bendi ya beta la muzika kutosa kupiga. siku hiyo wameanza kupiga nakumbuka alikua ni nyoshi,yule mpiga gita wao mfupii nimemsahau,na wengineo siwakumbuka walikuwa watano tu,kwa nini nimesema drum mchina?mpaka muda wanamaliza muziki saa sita usiku drum ilikua imetoboka mbaya,na gitaa kuna vinyuzi vilikatika na amlifier ilikua inatoa mkoromo wa kufa mtu.ila nitakachowasifia jamaa walipiga muziki safi sana jioni hiyo ingawa vyombo vilikua vinawaangusha.nakumbuka baada ya shoo hiyo niliulizwa we umeleta bendi gani hii?nikawaambia hii bendi ni nzuri sema tu sasa hawana vyombo na hawako wote.nakumbuka baada ya hapo tenda ya pili kupiga pale wakatoswa,nikawaleta twanga pepeta na choki,kipindi hicho banza kahamia T.O.T.na sikuwasikia tena fm mpaka siku moja nikawafuma bahari beach wakijifua vibaya baada ya kupata udhamini wa yule pedeshee (kibongobongo)chaula,na ndio toka walipotoka huko mazoezini,ndio ikawa fm academia ya ukweli na walikua wanachapa muziki balaa,na ndio wakazindua albamu yao wajelajela gwaa"PRISON".pale fm club kinondoni. toka hapo na walipopata mkataba na heineken beer ikawa ntolee mpaka leo.

No comments:

Post a Comment