Thursday 14 July 2011

UJUMBE WA ANONIMASI

MR ISAACKIN

jana baada ya kuingia katika blog yangu kuangalia kilichojiri,nikakutana na ujumbe huo chini

Anonymous said...
"(UMEPATA MPINZANI WA UKWELI DARSTOCKHOLM.BLOG HII YAKO WATAKUWA WANAANGALIA WACONGO..IMEKULA KWAKO NYAMBAFU)"

sasa haihitaji sayansi ya rocket kumjibu mtu kama huyu,na kwasababu nimepoteza muda leo kumjibu atapata majibu ya kiungwana kabisa.

unajua mitandaoni siku hizi kumeingiliwa na wendawazimu,sababu sikuona sababu ya huyu bwana anonymous kuja na kuanza kuandika comment kama hii hapo,na sio hii tu ni nyingi ambazo napata za matusi na nna uhakika ni huyo huyo mtu mmoja anayeandika
sometime huku ughaibuni watu wengine waanataka kupafanya kama vile tuko yombo vituka ama mbagara rangi tatu kwa mambo yao ya ajabu ajabu.mtu akishatoka kupiga box lake huko kashachoka kwa kupinda mgongo,karudi nyumbani kala ugali wake wa managryn na vibawa au hons hana kingine anachofikiria zaidi ya kutafuta computer iko wapi aingie kwenye mablog na kuanza kuandika ushuzi wake.maana hakuna jingine analojua zaidi ya kuwasha na kuangalia picha za kuuza sura katika blog na facebook basi.
hakuna faida nyingine ya ziada anayojua kuhusu computer ama hata blog.mtu wa namna hiyo akiingia kwenye blog akakuta kuna post ina maandishi marefu marefu anaipita maana anaona inampotezea muda,kumbe saa nyingine post hiyo hiyo anayoipita labda ina habari ya familia yake huko gong"s kupigwa mabomu,ama ajali inawahusu ndugu zake.yeye anachojua ni kuangalia picha kama katokea akiwa anauza sura kwa msanii diamond au ali kiba akitumbuiza basi anafurahiii ili awaonyeshe ndugu zake uko uswekeni kwamba yeye kawa maarufu stockholm.

sasa bwana anonymas,blog hii ni ya burudani kwa ujumla na sio blog ya kuonyesha habari za hitima,arobaini wala kuuzia sura,ukiona haikupendezi we hama kuna inaowafaa,na unapohama huna haja ya kuniaga kwa sababu hata ulipokuja hukugonga hodi sasa unakuja kuaga ili iweje?
unaaga kwani mimi mumeo ama mamaako kwamba ntakulilia?
we nenda hata hamia blog za matakoni maana akili yako imejaa miguu ya kuku sitashangaa hata huko ukaandika ufyolo wako ukasema unahama.
kuna blog mabilioni hapa duniani na watu wanahama na kuingia wapya kila siku,kama wangekua wanaaga kama wewe ingekuwaje?
wewe ukiona blog haikufai jikate ukatafute blog itakayokufaa au itakayokuweka ukiuza sura yako mbovu pale kungsgården,nafasi hiyo humu hakuna na naweka kile ntakachoona mimi kinafaa ikiwezekana anzisha blog yako ni bure tuu kisha andika hizo komenti za anonymas mpaka uchoke.

na bahati mbaya sana nimejua we ni nani hivyo ukiendelea na utumbo wako ntakuweka hapa hewani na comment zako zooote za majitaka unazomwaga humu.

blali-kukuz!

10 comments:

  1. Pole kaka Isaackin,kila kitu kina uzuri na ubaya,faida na hasara.Pamoja!

    ReplyDelete
  2. Mtandaoni kama tu URAIANI ni vigumu kweli kumtuliza kila mtu!

    Na kwa bahati mbaya inasemekana kwa kawaida KIBINADAMU hata mtu afanyaje huwa inafikia mpaka MKE aliye wahi kumpenda MME jana hata kindoa si kila siku ananogewa na hata adaicho na ajuacho ni kitamua,...
    ...
    ...kwa kuwa labda siye WANADAMU huwa haturidhiki na kukiwa na hiki huwa twadhania KILE ni kitamu!

    DUH naacha na ngojea moja kwamoja niangalie uwezekano wa KIMADA leo!:-(

    ReplyDelete
  3. asante sana da swahili siwezi kufikiria ubaya km mtu anipe ushauri tu kiungwana,sio matusi na kutisha kuhama,sijapangisha mtu hapa ye aende tu.
    bro simon nimekuelewa sana hawa ndio km wale wake vicheche kila anakoolewa anafikiria aende kwa muuza genge,au nyama au hata muuza utumbo mradi aachie uchi apewe utumbo wa bure hela aliyopewa na mumewe akachezee upatu
    its same here

    ReplyDelete
  4. watu hao wameenea sana kila pembe hapa mjini....stockholm.wala si kwa blog tu hata mtaani ukipendeza maneno ukichukiza maneno ukizishika pesa maneno ukiishiwa ndo dooooo utakuwa discussion.achana nao kaka isaack.hawapendi kuiona meli ya mtu baharini....na ndio cinderella yako ipo kati kati kazi kwao.......

    ReplyDelete
  5. CHONDECHONDE sina blog ila nakuasa ki2 ndugu yangu, hata siku moja usipoteze mda wako kuwajibu watu km hao unapoteza nguvu na muda MAJUNGU STCKHM ni ki2 cha kawaida kwa wake na waume we unachotakiwa unapoteza tu by the way mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe kwanini akwambie wewe wakati kuna blog nyingine km 3 ivi mjini hapa???NARUDIA TENA ISACK USIJIBU COMMENT HATA UTUKANWE na iyo anony uiache ili wazidi kuandika wewe unaamua kuiweka iyo comment au kuilia ganzi

    ReplyDelete
  6. Isack bwana ivi we majungu ya stckhlm huyajuai???na aloandika ni m2 wako kbs mi ndomana wakati mwingine sitaki marafiki wanawake na wanaume tunashindana kwa umbea.we kula ganzi usiwajibu. Jiwe linarushwa gizani ukisikia yalaaa ujue limempata m2 asa we kimyaa ili wazidi kurusha mana hata km ni mwanamke yule mwenye mvuto ndo mwenye kufuatwa sn japo kila m2 ana choice yake ila akipita lazima uisome

    ReplyDelete
  7. asante mdau ushauri wako umepokelewa,huwa sina muda wa kujibu comment za kipuuzi,ila imetokea baada ya kukaa kimya muda mrefu na mtu huyo kuendelea kusumbua na comment zake nyingi sijaziweka hapa

    ReplyDelete
  8. Pole kwa yaliyokukuta KIJANA,lakini hao wako wengi ukisema uwajibu ndio wanaongezeka.Wapotezee kama walivyosema wachangiaji wengine.

    ReplyDelete
  9. wapotezeeeeeeeeeeeeeeee.....kama alivyosema MDAU hapo juu.jiwe linarushwa gizani ukisikia mamaaaaa basi mtu kaipata.yaani wewe weka GANZI...funga kabisa vioo......umesavaivu mangapi bwana...wala hawatokuwa wamwisho.... donge tu...

    ReplyDelete