Friday 8 April 2011

HAYA MA-SHAROBARO MNAIJUA MAANA LAKINI?






WANAOJIITA MARAIS WA MASHAROBARO

MalkIA wa Mipasho Bongo, Khadija Omary Kopa, ameibuka na kusema kuwa, neno sharobaro ambalo limeenea mitaani ni tusi kubwa lenye maana ya mwanaume aliyelegea anayefanyiwa kila kitu.

Mwanamipasho huyo alifunguka hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuwa, anashangazwa na vijana wa kiume wanaojiita masharobaro huku wakiwa hawajui maana na asili ya neno hilo.

“Siku hizi eti kijana wa kiume anajigamba kuwa yeye ni sharobaro huku akiwa hajui maana halisi ya neno hilo. Ukimuuliza maana yake atakwambia ni mtu mtanashati anayejua kupangilia ‘pamba’.

“Ukweli ni kwamba, neno hilo linatumika Uarabuni kwa mwanaume ambaye hajishughulishi na kazi yoyote,  badala yake huzurura kutwa na watoto wa kike akisubiri afanyiwe kila kitu na dada au mama yake.

“Hata sauti yake akiongea utamuonea huruma jinsi alivyolegea,” alisema malkia huyo na kuwataka vijana kuacha kujiita jina hilo.

Hivi karibuni kumeibuka rundo la wanaume, hasa vijana kujiita masharobaro huku wakishindwa kujua maana halisi ya jina hilo.

Safu hii inafanya jitihada ya kujua ni kweli jina hilo lina maana aliyosema Hadija Kopa? Fuatilia matoleo yajayo

chanzo:GPL

HAYA VIJANA MSHAAMBIWA MAANA HASA YA HILO NENO MENGINEYO MTAMALIZIA WENYEWE,NA PIA MTAAMUA KAMA MUENDELEE KUGOMBEA PODA NA LIPSTIK NA DADA ZENU AMA MUACHE,NA VIDUME VIKIWATOKEA HUKO MITAANI MSIRUSHE NGUMI

No comments:

Post a Comment