Wednesday 20 April 2011

UGALI






kuna asiyependa ugali kwa sisi wamatumbi?wapo wasiopenda.
je ushawahi kula ugali na kitu gani cha ajabu?
MENU

ugali na chumvi
ugali na asali
ugali na maziwa
ugali na uji
ugali na supu
ugali na mlenda
ugali na maharage(hii kila mtu ashakula)
ugali na hamira (mmh wale wa mama ntilie)

lakini katika vyote hivyo uupate ugali kwa mboga yenyewe isiyo na mikwaruzo,ugali utaupenda.kuna wanaoshangaa kwanini tunapenda ugali,wao wanadai ugali hauna ladha maana hauungwi chumvi wala sukari,lakini nani ataacha kula ugali?tena waache wao wasiupende ili watuachie sisi kwa wingi maana wakiupenda wanaweza wakamaliza.
sasa kwetu kule vijijini singida ukute umepikiwa ugali na mboga inaitwa "sansa teleka" ama "mlenda" uliochanganywa na "majani ya maboga" hutatamani kumaliza.
au kule vijijini kwetu kwingine mbeya ukute umepikwa ugali na majani ya maharage"nguniyani"usifanye mchezo hiyo habari yake.
je wewemdau ushawahi kula ugali na nini mpaka  ukavimbiwa?

acheni habari ya ugali ibaki kuwa ugali,hizo pizza na pasta na baga na potatis wacha wale wenyewe tutaendelea kukamata ugali mpaka vichwa vitoe unga hatuachi.

5 comments:

  1. kaka Isaac ugali ndiyo mambo yote wangu!!!!lakini ni kweli unamboga zake,mimi napenda na bamia,dagaa,mboga za majani au mboga kavukavu si michuziiiiiii!!kaa makao wa kula nitakupostia kitu bamia na ugali!!!!!!!!!Asante sana!!!!!!

    ReplyDelete
  2. ww Rachel umeniwahi:-:( ...LOL kwani hata mia napenda kweli ugali bambia,ugali tembele,kisamvu na bila kusahau samaki wa kuchoma waliotiwa pilipili na chumvi weeeeeeeeeeeeee ...basi naacha

    ReplyDelete
  3. mimi napenda ugali na mboga ya mnavu uliyochanganywa na nyama na maziwa ya mgando pembeni

    ReplyDelete
  4. hapana chezea ugali wa tembele na dagaa, ugali na rosti ya kuku + kisamvu, ugali na samaki pembeni na mambogamboga...

    ReplyDelete
  5. ugali, mlenda na kipande cha papa au samaki wa kukaanga...

    ReplyDelete