Monday 18 April 2011

KASEBA ASTAAFU NGUMI BAADA YA KUCHAPWA NA MAUGO

hapa kaseba kashachoka na kuvua gloves kabisa


washabiki wa kaseba walipoona boss wao kachoshwa wakaingilia kulianzisha ulingoni


maugo akatangazwa mshindi


BINGWA wa kickboxing, Japheth Kaseba amesema ameachana na ngumi na sasa amewaachia mabondia Francis Cheka na Mada Maugo watambe watakavyo katika mchezo huo.

Kaseba ambaye juzi alipigwa na Maugo kwa ‘Technical Knockout (TKO)’ katika raundi ya saba baada ya pambano kuvurugika, alisema hakuna jambo la kushangaza kwani aliahidi kufanya hivyo endapo angetandikwa na bondia huyo.

Bondia huyo mara baada ya pambano hilo aliliambia Championi Jumatatu kuwa, vurugu zilizotokea alipopigana dhidi ya Francis Cheka zilimkera na hakutaka zitokee tena kwa Maugo, hivyo kitendo cha ghasia hizo zilizozuka ulingoni hapo na kudumu kwa dakika 14 zilitosha kutangaza rasmi kutandika daruga.

“Natangaza rasmi kustaafu ngumi na nimechukua uamuzi huu ili kuunusuru mchezo huu kufa na mimi nikaonekana kikwazo kwa kutoka kwenye kickboxing na kuja huku kuua ngumi,” alisema Kaseba.
toka:GPL

POLE SANA MKUBWA,NI BORA UTUNDIKE DALUGA KULIKO KUADHIRIWA KILA SIKU NA VIJANA MWISHO WATAKUUA,HUO UAMUZI MZURI.

No comments:

Post a Comment