Monday 16 August 2010

SAFARI YETU MBEEYA TULIFURAHI SANA.


stesheni kuu ya treni maeneo ya iyunga mbeya,ushafika?


hii ndio round about ya mji wa mbeya,ukienda mbele unaelekea sokomatola.ukikunja kushoto unaelekea maeneo ya mabatini,ukipandisha juu kunaitwa uhindini,uzunguni,na huku unapotokea ni maeneo ya mwanjelwa au upande wa uwanja wa sokoine,jogoo rafiya huko bado naikumbuka toka nitoke miaka 22 sasa.

haka kamlima sitakasahau,kapo maeneo ya mjini enzi hizo al-maarufu kwa jina la sombrelo,hapa pahala ndipo baba yangu alipotutoka rasmi duniani baada ya kupata accident mbaya ya tuk-tuk na kufariki hapo hapo ilikuwa usiku wa february 16 1988.jina lake likabadilishwa na kuitwa R.I.P.NAZARETH MWAMUGOGWA.mungu amlaze pema peponi.
haya maeneo ya stand kuu ya mabasi mbeya.
eeh usipitishe haraka haraka ukafanya kama hujui,ushawahi lala ndani humo??sasa ukitaka kupata raha asili ya usingizi ni humo ndani,ka-apartment full A.C.halafu kako well funished na heater ya kufa mtu(moto wa kuni)ambayo haina bill.pia kama wewe ni mvuta fegi humo utabloo maana kuna full service ya moshi mda woote,na wala usiwe na shaka ya matress,hapo utapata tena zile orijino kabisa (sio za mchina)a.k.a( mikeka).huku permanent(walk by) toilet umbali wa mita 500,(nop kule hatuitaji kukaa na toilet ndani eti munaita (selufu kontena).pia utapata full toilet paper asilia (gunzi) ama (kuburuza mat..o chini kwenye udongo).na wakati wa kujisaidia usisahau kuangalia usalama wako,maana snake hawachelewi kuja kukuuliza hela ya kutumia choo.(na ole wako usilipe).ukimpeleka blonde wako huko hachelewi kukataa kurudi kwao(sijui kama kweli).kwa booking nione mimi.
mchuma wetu wa kuelekea huko kusini mbeya treni ya tazara(luxury)

wow,aliyesema mbeya hakuna beach nani?sasa hiyo ndio beach yetu kule(MATEMA BEACH)hapo utaogelea na bila kusahau samaki watamuuu na mpunga wa kyela.KARIBUNI MBEYA.

No comments:

Post a Comment