Sunday 8 August 2010

MISHKAKI LEO KATIKA MISOSI-MISOSI

Vipimo:

Nyama steki 4 Ratili (2 Kilo)
Mafuta 3 Vijiko vya supu
Masala Ya Kuroweka Katika Nyama:

Thomu na tangawizi iliyosagwa 2 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu

Siki nyeupe 3 vijiko vya supu
Chumvi kiasi

Jiyrah (cummin powder/bizari ya pilau) 1 kijiko cha supu

Dania (coriander powder/gilgilani) 1 kijiko cha chai

Pilipili nyekundu ya unga 1 kijiko cha supu

Mdalasini wa unga 1 kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika:

1. Kata nyama vipande vikubwa kubwa kiasi .
2. Changanya masala na vitu vyote katika nyama uroweke kwa muda wa masaa mawili.
3. Tunga vipande vya nyama katika vijiti vya kuchomea kababu (kabaab skewers).
4. Choma katika jiko la makaa au katika la B.B.Q kwa moto wa kiasi ukiwa unazigeuza geuza hadi nyama iwive.
5. Epua, weka katika sahani ikiwa tayari kuliwa.

N.B.waweza jaribu home siku hauko busy sio ngumu kabisa mie jana nimetengeneza na nikajinoma

No comments:

Post a Comment