Wednesday 11 August 2010

MKALI WA MASONGI KING-BLAISE AZICHAPA NA WIFE

Mwanamuziki tegemezi wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Mohamed King’ombe ‘King Blaise’ hivi karibuni alifikwa na mazito baada ya mkewe, Diana kulipiga ‘stop’ penzi lao kufuatia wawili hao kunyukana ndani ya ukumbi, kisa kikisomeka kama ‘fumanizi’ flani, Ijumaa Wikienda lina mzigo wote. Ndondi hizo zilijiri Ijumaa iliyopita ndani ya ugwa wa Mango Garden jijini Dar es Salaam na kuburuzana kwa takribani dakika thelathini mpaka kwenye Kituo cha Polisi cha Garden kilichopo karibu na ukumbi huo lakini baadaye wakarudi Mango. Baadaye wakiwa nje ya ukumbi huo huku wamekunjana, ndipo mwanamuziki aliyewahi kutamba na Bendi ya Diamond Sound, Allain Mulumba Kashama alitokea na kuingilia kati kusuluhisha ‘vita’ hiyo kwa kuwataka wawili hao kwenda kuyamaliza mambo yao nyumbani. Hata hivyo, Kashama hakufua dafu kurejesha amani kwa wanandoa hao, hivyo alimwomba mwanamuziki mwenzake wa Diamond Musica, Mulezili Boyange ‘Mulemule FBI’ amsaidie. Naye FBI alilazimika kutumia lugha zaidi ya tatu kikiwemo Kilingala, baada ya Kiswahili na Kifaransa kudunda na ndipo wawili hao walitulia huku mwanamke akitoa tamko la ‘kustopisha’ penzi lake kwa mwanamuziki huyo. Baada ya kutulia wote wawili waliingia kwenye gari moja aina ya Toyota Colora yenye namba za usajili Z 272 BN huku King Blaise akiweka kweupe kwamba, wanakwenda kuyamaliza wenyewe nyumbani kwao, Sinza. Akizungumza na Mwanahabari Wetu kabla ya kuondoka, King Blaise alisema yeye alitoka kutumbuiza na bendi yake Viwanja vya Karimjee, jijini Dar na mkewe aliaga anakwenda kwenye harusi ya mdogo wake (hakutaja sehemu), “lakini nashangaa kumkuta hapa Mango usiku huu wa manane,” alisema Blaise hali iliyotafsirika kuwa ni ‘fumanizi’. Kwa upande wake, Diana alishindwa kuweka wazi kwa Paparazi kisa cha timbwili kufuatia kuvuja damu nyingi mdomoni huku tai ya mumewe ikiangukia mgongoni badala ya tumboni.
SOURCE:GPL
sijui mke kweli au ndio wale wale wa kupewa maisha na mijimama kibongo-bongo.ukikuta wenyewe wanaogharamia wanakaba unaanza kurusha ngumi.

2 comments:

  1. nice king blaise is the best

    ReplyDelete
  2. she has a canadian woman now i dont know what will happen next

    ReplyDelete