Thursday, 6 September 2012

OMMY DIMPOZ KUZINDUA VIDEO YAKE BAADAE JUMAPILI
MSANII wa Mziki wa Kizazi kipya anaetamba na nyimbo zake mbili za Nai Nai na Badaye, na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz anataraji kuzindua Video yake mpya ya Baadaye katika ukumbi wa Club Maisha Septemba 9,2012 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Father Kidevu Blog, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika naya kuvutia.

Mubenga amesema Omy Dimpozy ameifanyia shooting video yake hiyo nchini Afrika Kusini. 

Aidha Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa vuideo hiyo ulifwanywa na Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri nae hadi Afriia Kusini na wameshoot kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.

“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga. 

Amesema wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa video hiyo mpya na Dimpoz nae atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliye mzoea.

Pia Meneja huyo wa Omy Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika kusini Dimpoz alimshirikisha Model ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi wakali wa Mziki nchini humo anaejulikana kwa jina la Tully Tshabalala. 

“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya Televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.

Mubenga amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club Maisha Oyster bay jijini la Dar es Salaam jumapili.

No comments:

Post a Comment