Friday, 7 September 2012

UNAWAKUMBUKA EXTRA MUSICA-WAONE HAPA LIVE
he he hee,naona hapo mwanzo mwanzo kuna wazee wa pamba huko wanajiita (KING LE SAPPEUR)wamevamia ukumbi na suti zao kali kali mianvuli,bakora na cigar zisizowashwa milele ndio swagga zao ,kuna mmoja tunae hapa Stockholm taswira zake ninazo.

nawakumbuka hawa jamaa enzi hizo waliwahi kutua bongo wakawasha moto vibaya sana pale diamond jubilee,nakumbuka nilikua ndani siku na kuna kioja kilitokea pale baada ya dada mmoja kwenda kwenye stage na kusaula nguo karibia zote akimtaka rapper wa bendi hiyo anayejulikana kama KILLER MBONGO amfanye anavyotaka(haijambo).bahati mbaya sana killer mbongo kashatimka humu kundini lakini bado kuna rapper mwingine mpya ZAPPARO anapiga kazi  moto ni ule ule.waone live hapa mdau kuna solo linacharazwa humu ndani na seben lao si la kupima.hapa zimepigwa nyimbo kali kali kama zangul na matongi na nyingine kibao.

week end njema!

No comments:

Post a Comment