Tuesday 11 September 2012

USAFIRI WA TRENI DAR KATIKA MAJARIBIO

                                            Treni hiyo ikiwa tayri kuanza safari ya majaribio

                                               abiria nao hawakuwa nyuma kuona majaribio hayo
                                                                  kitu hicho kinapiga masafa


watu wakiwa na furaha kwa kuona huduma hiyo inakaribia kuanza,behewa safi,siti safi zimewekwa,kwenye kusifia tusifie at least kuna kitu kimeongelewa na wanasihasa na kikatekelezwa kwa muda mfupi.tunasubiri kwa hamu kuanza huduma hiyo

Usafiri wa treni jijini Dar es saklaam utaanza mwezi Oktoba baada ya kukamilika kwa maboresho ya reli kutoka Ubungo hadi stesheni.

Akizungumza jana baada ya kufanya safari ya majaribio Naibu waziri wa Dk Charles Tizeba alisema kufikia mwezi ujao treni hyo ityaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi waishio maeneo inapopita treni hiyo.

“Kufika Oktoba tutakuwa tumeanza kutoa huduma maana leo tumeanagalia uwezekano na tumeona tunaweza ufanya huduma na kurekebisha kasoro zilizobaki” alisema Dk Tizeba .

Dk Tizeba alisema kuwa reli hiyo kwa sasa bado haijakaa vizuri hivyo inahitaji kurekebishw aili trenio hiyo iwee kwenda kasi zaidi na kubomolewa kw anyumba zilizojengwa jirani na reli hiyo.


“Inashangaza sana kwani kuna watu wamejenga nyumba zao jirani kabisa na reli na wengine wamediliki kujenga mita moja kutoka relini, hii inahatarisha maisha yao wengyewe na hata wasafiri watakaotumia ttreni”


Hivyo alisema kuwa tayari watu hao wametaarifiwa juu ya kuondoka katika maeneo hayo na kwamba watatakiwa kuvunja wenyewe na wakikaidi basi watavunjiwa ili huduma hiyo ianze kutolewa.



Chanzo: www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment