Friday 19 October 2012

HOSPITALI YA MISSION YA IGOGWE YATIMIZA MIAKA 50 YA JUBILEE.



 Baba Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mbeya Evaristo Chengula, akimwagia maji ya baraka mnara wa jubilei ya kutimiza miaka 50

Maandamano ya ya maadhimisho ya miaka 50 ya hospitali ya igogwe yalianzia hospitalini hapo
Brass bendi ya chuo cha magereza kiwila wakiongoza maandamano hayo






Kwaya mbalimbali zilikuwepo kutumbuiza katika maadhimisho hayo



Mkuu wa Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela.
ambae alimuwakilisha mkuu wa mkoa mbeya katika maadhimisho yahyo







Mzee wa kinyakyusa akionyesha jini ya kucheza ngoma ya kabila hilo



Hospitali ya Mission ya Igogwe iliyopo Kata ya Kinyala, Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya imeadhimisha jubilee ya miaka 50 tangu kuanza kutoa huduma ya matibabu mwaka 1962 na sherehe hizo kufikia kilele chake Oktoba 18 mwaka huu.
Hafla hiyo iliongozwa na Baba Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mbeya Evaristo Chengula, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ambaye katika sherehe hiyo aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya Rungwe ndugu Crispin Meela.
Katika hotuba yake Baba Askofu ameiomba Serikali kufanya haraka kutoa eneo la ardhi ili hospitali hiyo iweze kupanua shughuli zake ikiwa ni pamoja kuanzisha Chuo cha Wauguzi ili kuisaidia Serikali katika uboreshaji wa sekta ya Afya nchini.
Askofu Chengula amesema Kanisa la Kikatoliki lina nia ya kuleta maendeleo zaidi katika hospitali hiyo licha ya wananchi 9 kugoma kuachia maeneo yao ili kupisha ujenzi wa majengo ya hospitali kwa ajili ya chuo na mahabara ya kisasa.
Aidha uongozi wa hospitali hiyo ulimweleza mgeni rasmi kuwa zaidi ya watu 150,000 hupatiwa huduma ya malazi kwa mwezi na kwamba zaidi ya wagonjwa 400,000 hutibiwa na kurejea makwao.
Vilevile hospitali hiyo imelenga kutoa ajira kwa watumishi 120 wa kada mbalimbali wakiwemo madaktari, wauguzi, mafamasia na kada nyingine na kwamba kila mmoja waweze kuifikisha hospitali hiyo ambapo kwa mwaka imeweza kuhudumia zaidi ya wagonjwa 5600 na huduma ya upasuaji kwa wagonjwa zaidi ya 503.
Hata hivyo  hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa wafanyakazi wa kada mbalimbali na uongozi umeitaka Serikali kuongeza watumishi, kwani hospitali hiyo imekuwa ikitoza kiasi kidogo cha fedha, hali iliyopelekea kuwa kimbilio kwa wananchi wengi kutoka mikoa ya Rukwa, Iringa na Ruvuma pia nchi za Zambia na Malawi kutokana na ubora wa huduma unaotolewa na hospitali hito.
Wakati huohuo hospitali inakabiliwa na changamoto za upungufu wa vitanda, ambapo hivi sasa kuna vitanda 140 za kulaza wagonjwa katika wadi tano zilizopo, ukosefu wa gari la kubebea wagonjwa, ulipaji wa mishahara kwa wakati, pesa za kulea watoto wanaokaa katika mazingira hatarishi na hawajiwezi, ukatikanaji wa umeme na barabara mbovu ambayo huweka adha kwa wagonjwa pindi wanapokimbizwa katika hospitali hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bwana Crispin Meela amesema ombi la ardhi litaanza kufanyiwa kazi Oktoba 22 mwaka huu na suala la barabara atawasiliana na wakala wa barabara nchini(TANROADs), ili baada ya hiyo iingia katika mpango wa mkoa ili kuboresha miundombinu katika hospitali hiyo na kwamba barabara hiyo yenye urefu wa Kilimita 4 iwe lami.
Askofu Chengula amewashukuru wafadhili waliolazwa katika Hospitali hiyo na pia anaomba ruzuku ya madawa katika bohari ya serikali(MSD) huku huduma za watu wanaoishi na VVU, pia huduma ya mama na mtoto ambayo ilipaswa kutolewa na serikali.
Mbali na sherehe ya Jubilee Askofu Chengula alizindua mnara rasmi wa Jubilee hiyo na kuwapa daraja la kipaimara vijana na wazee wapatao 200 katika sherehe iliyofana na kuwataka waeende katika maadili yatakayompendeza Mungu na wanadamu pia nao kuleta amani na upendo kwa waumini na wasiokuwa waumini kwani kumekuwa na matukio ya uhalifu ambao wengi hufanya na watu waliopata kipaimara hivyo vijana wasifurahie tendo hilo tu bali wafuate Mema kwa kristo.


Habari na Ezekiel Kamanga, Rungwe

No comments:

Post a Comment