Wednesday 10 October 2012

Uchumi wa dunia watetereka zaidi

Sarafu za ukanda wa Euro
Shirika la fedha duniani IMF linasema kuwa kumekuwa na vikwazo vipya katika kujaribu kuunusuru uchumi wa dunia .
Shirika hilo linasema kuwa halina matumaini makubwa kuhusu kuchepuka kwa uchumi wa dunia na linatarajia uchumi wa kanda ya Euro kuanguka zaidi kwa asilimia nusu mwaka huu.
Katika ripoti yake mpya shirika la IMF linasema tatizo kubwa ni kwamba sera za uchumi katika nchi zilizoendelea zimeshindwa kujenga upya imani ya ukuwaji wa uchumi .
IMF sasa imeshusha viwango vyake vya matarajio ya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa kiwango cha asilimia tatu kwa mwaka huu na mwaka ujao na kusema kuwa matumaini ya ukuwaji yatakuwa juu mwaka ujao.
Limesema kuwa sera katika nchi zilizostawi, zimekosa kujenga matumaini na hivyo kusababisha hali ya taharuki katika masoko ya Ulaya.

BBCSWAHILI

No comments:

Post a Comment