Tuesday, 30 October 2012

Hukumu ya Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira kusomwa leo


 
Hukumu ya Kesi ya mauaji ya Marehemu Swetu Fundikira inayowakabili askari jeshi Sajent Rhoda Robert, Koplo Ally Ngumbe na Mohamed Rashidi inatarajiwa kusomwa leo Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es salaam.

Washtakiwa hao watatu wanadaiwa kuwa siku ya Jumamosi tarehe 23 Januari, 2010 walimpiga bila huruma Swetu Fundikira katika maeneo ya Kinondoni katika makutano ya barabara  za Mwinjuma na Kawawa jijini Dar es salaam mpaka kusababisha kifo chake.

No comments:

Post a Comment