Friday, 19 October 2012

NAZIMISS HIZI HATUA TATU ZA NYAMA CHOMA

KWANZA NIPALE UNAPOFIKA KWENYE NYAMACHOMA UNAIKUTA IKO JIKONI LIVE INACHOMWA TARATIIBU,UNAAGIZA KISHA UNAENDA KUKAA KUSUBIRI IKAMILIKE HATA IKICHUKUA MASAA MAWILI UNAISUBIRI NA KA NDOVU BARIIIIID(NO HURY IN AFRICA).HATUA YA PILI NI PALE INAPOKATWA KATWA NA MCHOMAJI HUKU AKIHAKIKISHA ANAWEKA SIZE INAYOFAA USIKABWE MAANA KUNA WENGINE WANATAKA KUFAKAMIA KAMA WAKO KWENYE OLYMPIC YA KULA
 NYAMA
 
 HATUA YA TATU NI PALE SINIA LINAPOTUA MEZANI KAMA PICHA INAVYOONYESHA,HAPO UNAKUA TAYARI UNA HAMU MAANA BIA KADHAA ZIMESHUKA KUKUPA APETITE YA KUTOSHA

 
 KWA WENGINE TUNAOPENDA NA UGALI NDO KAMA HIVI,ILA WENGINE WANAONDOKA KAVU KAVU NA NYAGI INAENDA MUKIDE TUU!

WATAALAM WA KUCHOMA HII KITU UKALA UKAISHIWA HAMU MARA NYINGI JIONI NILIKUA NATEMBELEA PALE KONA BAR SINZA.
NJE PARKING SIKU HIZI KUNA WACHOMA NYAMA KAMA WATANO HIVI WANACHOMA NYAMA YA KILA AINA FRESH YA KUTOSHA LAINI NA INA LADHA SAFI KABISA,
WADAU HASA MLIOKO UGHAIBUNI MKIFIKA BONGO MKALETA USHAROBII KULA MAHOTELINI SHAURI YENU,MI NILIKUA NASHINDA HUKU MAFICHONI MITAANI NIKIAGIZA NYAMA YA 15,000 SIMALIZI.
WAKATI HUKO MNAENDA MASAKI MAHOTELINI HIYO NI HELA YA MSHKAKI MMOJA BILA KIEPE,HAPO TUSAMEHEANE HUKO MI SIENDI BANA NTASHINDA HUKU HUKU USWAZ,MAANA MAENEO HAYA SI UNAJUA TENA NA WALE "KUKUWETU WA KIENYEJI"HAWAKOSEKANI AROUND,PIA UKIKUTANA NA HAO KUKUZ HATUIMBIANI NYIMBO ZA KINA CHRIS BROWN,KISHA TUPIGE STORO ZA BBM NA FESIBUKU AKHA!

HAPO UKUTANE NA KUKU WAKO MNASHIRIKIANA HIYO NYAMA NA BIERE NA NYAGI BAADAE MNAANZA KUITANA "MAI LAVU,MAI LAVU" KISHA MAKISS KIBAO,MARA INAKUA ADIOOOS AMIGOOOZ!

WEEK END NJEMA WADAU

No comments:

Post a Comment