Mwandishi wa Habari wa Radio
France International (RFI Kiswahili) Bw. Ali Bilali akifanya mahojiano
na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini
(UNDP) Bw. Phillippe Poinsot (kushoto) ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya
miaka 67 ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Wetu
Umoja wa Mataifa umeanza kuadhimisha
wiki mahsusi kwa ajili ya Umoja huo kwa kufanya shughuli mbalimbali
ambapo nchini Tanzania taasisi za Umoja wa Mataifa, Serikali ya Tanzania
na mashirika ya kiraia wanakutana kuzungumzia maswala mbalimbali
yahusuyo maendeleo, utawala bora na njia za kupiga vita umaskini
uliokithiri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la
Umoja wa Mataifa linalohusika na Maendeleo nchini Tanzania UNDP
Philippe Poinsot, amesema Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa
Mataifa ambayo inawajibika vizuri kwenye umoja huo.
Mbali na hayo Mkurugenzi huyo wa UNDP
amesema kuwa Umoja wa Mataifa unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza
umasikini uliokithiri nchini Tanzania ambapo takriban dola za Marekani
lakini nne milioni hutolewa katika kipindi cha miaka minne.
Wiki ya Umoja wa Mataifa imeanza kuadhishwa Oktoba 17 na itafikia kilele Oktoba 24 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment