Friday, 19 October 2012

NENO LA MWISHO LA KAMANDA BARLOW KWA MKEWE

Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini…
Na Sifael Paul
HUKU mumewe akiwa amezikwa Jumatano iliyopita kijijini kwao Kilema, Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, mke wa aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow (53), aliyeuawa na watu waliosadikiwa kuwa ni majambazi wiki iliyopita, amefunguka neno la mwisho alilozungumza na baba watoto wake huyo kabla ya kukutwa na umauti, Ijumaa linakujuza.
Mjane wa Marehemu Liberatus Lyimo Barlow, Stela Lyimo akiweka shada katika kaburi la mumewe.
Akizungumza na kituo kimoja cha redio cha jijini Dar es Salaam, juzi huku akiangua kilio kwa uchungu, mke huyo wa marehemu ambaye walijaliwa watoto watatu alisema kuwa mara ya mwisho mumewe alimwambia kuwa anakwenda kwenye kikao cha harusi ya ndugu yao na hayo ndiyo yalikuwa mazungumzo yao ya mwisho.
Huku akishindwa kuzungumza vizuri kutokana na maumivu ya kuondokewa na mwenza wake huyo, mama huyo alisema maneno hayo ndiyo yalikuwa ya mwisho kuzungumza na muwewe hadi alipopata taarifa ya kifo hicho ambapo mwanzo ilikuwa vigumu kuamini.
Alisema kwa upande wake anaamini serikali kupitia Jeshi la Polisi nchini itafanya kazi yake hivyo hakutaka kuongeza neno kwani uchunguzi wa mauaji hayo unaendelea na kila kitu kitajulikana utakapokamilika.
Kamanda Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 13, mwaka huu eneo la Kitangiri, Mwanza kwa kupigwa risasi na watu hao waliokuwa wamevaa  w w makoti yanayovaliwa na vijana wa ulinzi jamii.

gpl

No comments:

Post a Comment