Thursday, 25 October 2012

DALLAS WA WOLPER AMNYANG’ANYA GARI BOB JUNIOR

TAA wa Bongo Fleva, Raheem Nanji ‘Bob Junior’ amenyang’anywa gari aina ya Toyota Mark II na zilipendwa wa mwigizaji Jacqueline Wolper, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
Sosi wetu alisema: “Unajua Bob Junior ndiye aliyefanikisha Dallas kumpata Wolper, sasa baada ya wawili hao kumwagana ndipo jamaa akaamua kulichukua gari lake kwa Bob Junior.”
Raheem Nanji ‘Bob Junior’
Dallas alipopatikana na kuulizwa alikiri: “Lile gari ni mali yangu, nilimpa atembelee kama ndugu na pia asante kwa kazi aliyonifanyia (hakuitaja), sasa nashangaa watu wanaongea sana mimi kulichukua gari langu.”
Bob Junior yeye alipopatikana, alikuwa na haya ya kusema: “Kweli gari lilikuwa mali yake lakini kuna kipindi wakati yupo Ulaya alinikopa fedha kwa kuliweka bondi hilo gari na aliendelea kunikopa hadi kufikia milioni 9, ikabidi nimwambie aniuzie tu gari ili tumalizane.
 

Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
“Lakini hakuwa tayari kufanya hivyo sasa juzi nikashangaa anakuja na kusema nimmalizie fedha za gari ana shida, sikuwa tayari kumpa, nikamwambia amtafute mteja amuuzie gari anilipe pesa zangu na yeye achukue zitakazobaki, lakini akaondoka na gari hadi leo hii (Jumapili iliyopita) sasa sielewi kama kaliuza au vipi, ila kadi ya gari ninayo mimi na siwezi kuitoa hadi anilipe fedha zangu.”

gpl

No comments:

Post a Comment