Usafiri wa Treni Dar es Salaam Wanza Rasmi Leo
USAFIRI wa
kutumia treni jijini Dar es Salaam kutokea eneo la Ubungo Maziwa
kuelekea katikati ya Jiji la Dar es Salaam (Stesheni ya Treni) umeanza
leo. Treni ya kwanza imeondoka Ubungo majira ya saa 12:00 asubuhi
kuelekea katikati ya jiji, ambapo kwa mujibu wa maofisa wa Shirika la
Reli Tanzania (TRC) imetumia wastani wa dakika 30 kufika katikati ya
jiji.
Treni
ilioanza kazi leo iliyokuwa na injini mbili (vichwa vya traini) moja
ikiwa imefungwa nyuma na nyingine mbele huku ikiwa na mabehewa sita,
yaani matano ya abiria wa kawaida (watu wazima) na moja likiwa ni
maalumu kwa ajili ya kubeba wanafunzi. Abiria mmoja ni sh. 400 kwa tripu
huku wanafunzi wakitakiwa kulipa sh. 100 kwa kila mmoja.
Waziri wa
Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ndiye aliyezindua usafiri wa leo ambao
ni wamajaribio, akiwa pamoja na viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka
ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi
Kitengo cha Reli.
Treni hiyo
pia imezinduliwa pamoja na treni ya TAZARA ambayo itafanya kazi kama ya
Ubungo, lakini yenyewe ikianzia eneo la TAZARA kuelekea Mwakanga.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi huo Waziri Mwakyembe alisema
atahakikisha treni hiyo inaendelea kufanya kazi ili kuwasaidia kiusafiri
wananchi wa Dar es Salaam ambao wamekuwa wakisumbuliwa na kero ya
usafiri hasa kwa foleni, ambapo utumia muda mrefu njiani kuingia na
kutoka jijini.
Alisema
jumla ya mabehewa ya treni 14 pamoja na injini mbili zimekarabatiwa na
mafundi wazalendo nchini, ambayo ndiyo yatakayokuwa yakifanya kazi ya
kusafirisha abiria kuingia na kutoka jijini kila asubuhi na jioni.
Alisema kwa sasa inafanya treni moja kwa majaribio lakini baada ya
uzinduzi mkubwa zitafanya kazi treni mbili, na zitakuwa zikipishana
njiani moja ikirudi na nyingine ikienda.
Akifafanua
zaidi alisema kitendo cha mafundi wazalendo kufanya ukarabati kwa
mabehewa na injini kimeokoa kiasi kikubwa cha fedha za umma kwani
ukarabati wote umetumia sh. bilioni 2.1 tu, ilhali kama Serikali
ingelazimika kukodi injini gharama ingekuwa kubwa zaidi kwani bei ya
kukodi injini moja ya treni ni sh. milioni moja kwa siku.
Hata
hivyoDk. Mwakyembe amewataka Watanzania hasa abiria kuwa wavumilivu kwa
upungufu utakaojitokeza kwa safari za mwanzo kwani bado wanaendelea
kufanya marekebisho kadhaa, lakini baada ya muda mambo yatakaa sawa.
Mwandishi
wa habari hizi alikuwa ni mmoja wa wasafiri walioizindua treni hiyo leo.
Awali akizungumza mmoja wa viongozi waandamizi wa TRC, alisema treni
hiyo itafanya kazi kila siku isipokuwa kwa siku za jumapili na siku kuu
na itaanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa sita mchana na kupumzika hadi saa
9:00 za jioni, itakapoendelea tena na safari zake hadi majira ya saa
nne usiku.
Uchunguzi
uliofanywa na muandishi wa habari hizi umebaini kuwa behewa moja la
treni linauwezo wa kuchukua abiria 66 wakiwa wamekaa, lina milango
minne, feni, taa, muziki/redio, pamoja na mikanda maalumu ya kujishikia
kwa abiria ambao watakuwa wamesimama.
Aidha mabehewa yote yana madirisha ya kutosha kuingiza na kutoa hewa ya
kutosha.
Treni
ilioanza kazi leo, ikitokea Ubungo ilikuwa ikisimama vituo vya eneo la
Mwananchi (relini), Tabata Relini, Buguruni Miamani, Tazara, Kariakoo
Gerezani (Kamata), na mwisho Kituo Kikuu cha Treni kilichopo jirani na
Kituo cha Polisi Kati (Katikati ya Jiji).
Abiria wa Usafiri wa Treni uliozinduliwa rasmi leo kwa ajili ya safari za ndani ya Jiji la Dar wakipanda usafiri huo.
Abiria Wakisubiri Treni Kituoni.
Treni ikiwa safarini.
Abiria
wakiwa ndani ya Usafiri wa Treni huku wengine wakiendelea kupata nyuzz
mbali mbali tena kwa utulivu kabisa kupitia magazeti.
Tangazo la Usafiri huo wa Treni.
Abiria ndani ya Treni
Abiria
wakiwa wamejitokeza kwa wingi kupanda Treni zinazofanya usafiri wake
ndani ya jiji la Dar mara baada ya kuzinduliwa rasmi leo na Waziri wa
Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe.
Treni ikichanja mbuga.
Abiria wakiwa ndani ya Treni hiyo huku wakiwa ni wenye furaha na usafiri huo.
Wakaguzi wa
tiketi za Treni wakiwajibika mchana wa leo wakati wa Uzinduzi wa Safari
za Treni ndani ya jiji la Dar es Salaam mara baada ya kuzinduliwa rasmi
leo na Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na baadhi ya viongozi waandamizi kutoka TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es Salaam mapema leo.
Waziri wa
Uchukuzi,Dk. Harrison Mwakyembe akiwa nadni ya treni hiyo sambamba na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi pamoja na viongozi waandamizi kutoka
TRC, Mamlaka ya Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), TAZARA pamoja na Polisi Kitengo cha
Reli wakati wa uzinduzi wa Safari za Treni ndani ya Jiji la Dar es
Salaam mapema leo.
habari na picha-matukiomichuzi
No comments:
Post a Comment