Thursday, 25 October 2012

VIONGOZI UAMSHO WARUDISHWA TENA RUMANDE

 Mawakili wa Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Abdallah Juma kushoto na Salim Tawfik wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu nia yao ya kujitoa kwao siku ya leo katika kesi hiyo kutokana na kile walichoita  usumbufu wanaofanyiwa wateja wao wa kuhangaishwa na kukosa kupelekwa Mahakama ya Kwerekwe kwa muda muafaka 
 Kiongozi wa Jumuiya ya UAMSHO Sheikh Farid Hadi Ahmed kushoto akiwa na wenzake sita walioletwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga wakiwa hawana ndevu na kufunguliwa mashtaka manne mapya mahakamani hapo yakiwemo kuharibu mali za watu zenye thamani ya Shl.Milioni 50 na kufanya vurugu za makusudi zakuhatarisha amani katika nchi
 Baadhi ya Askari wa kutuliza fujo wakiwa Mahakama kuu Zanzibar Vuga kwa lengo la kulinda usalama na  amani Mahakamani hapo
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya ya UAMSHO wakiwa wanatoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar Vuga baada ya kufunguliwa mashtaka manne mapya..Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

No comments:

Post a Comment