Saturday, 13 October 2012

PICHA ZA ENEO LA TUKIO ALILOPIGIWA RISASI KAMANDA BHALOW NA MAELEZO YA KILICHOTOKEA KABLA HAJAUWAWA

 Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Everest Ndikillo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusiana na tukio la kifo cha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Liberetus Ballow usiku wa Kuamakia leo maeneo ya Kitangiri.
           Hapa akijibu swali.
 Nyumba ya Dorcas Moses mwalimu wa shule ya Msingi ya Nyamagana ambaye alikuwa kwenye gari aina ya Rav 4 aliyopewa lifti na kamanda Ballow usiku kumrudisha kwake. Hapa Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Fredrick Katulanda akitoka kufanya mahojiano.
 Mtoto wa kaka yake Mwalimu Dorcas akiongea kuhusiana na tukio la Kifo cha kamanda Ballow ambapo yeye ndie alikwenda kufungua geti kwa ajili ya Mama yake Dorcas aweze kuingia ndani ila kabla ya kufungua ndipo aliposikia risasi ikipigwa.
          Hapa ni nyumbani kwa marehemu kamanda Ballow.
 Hili ndilo geti ambapo kifo cha kamanda Ballow kilipotokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Moses alipokuwa akirudi nyumbani kwa lifti ya gari la Kamanda Ballow.
   Baadhi ya jamaa yake marehemu wakiwa nyumbani kama walivyokutwa na kamera yetu.
                 Jamaa zake marehemu Ballow.
                   Waombolezaji wa kike wakilia kwa uchungu nyumbani kwa kamanda Ballow leo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Ballow ameuwa usiku wa kuamkia leo na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi katika eneo la Kitangiri karibu na Hotel ya Tai Five majira ya kati ya saa saba hadi nane.
 
Haya  yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Injinia Everest Ndikillo wakati akitoa taarifa za tukio la kuuawa kwa Kamanda Ballow.
 
Tukio hilo ambalo limeacha simanzi kubwa kwa wakazi wa jiji la Mwanza pamoja na familia yake huku watu wakijiuliza kuhusiana na aliyehusika na mauuaji hayo ya kikatili.
 
Taarifa ya Mkuu wa Mkoa zinasema kuwa Kamanda Ballow alikuwa anatoka katika kikao cha harusi na ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kinafanyika katika Hotel ya Florida na kishakumpeleka mwanamke aitwaye Dorcas Moses Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Nyamagana maeneo ya barabara ya Kona ya Bwiru kwenda Kitangiri.
 
Walipofika getini kwa Mama Dorcas mara waliwaona watu wawili wakiwa wamevaa makoti ya PolisiJamii, Mama Dorcas alimuuliza Kamanda Ballow kama anawafahamu Kamanda akasema kuwa hawa ni watu wa ulinzi Jamii wako doria.
 
Mara wale watu waliongezeka na kuwa sita wakaanza kama kuzozana wao kwa wao na  ndipo Kamanda alipowauuliza kuna nini, Mmoja wao akajibu hakuna kitu na ikapelekea Kamanda kutaka kutoka nje ila wale watu watatu wakaizingira gari ya Kamanda Ballow aina ya Rav 4.
 
Kamanda Ballow alipoona kama hali ya hewa inabadilika alichukua redio call ili aweze kuwa taarifu askari na ndipo wale jamaa walipompiga risasi kichwani nakupelekea kifo chake.
 
Taratibu za mazishi ya Kijeshi bado zinaendelea nyumbani kwa marehemu ambapo mwandishi wa blogu hii amefika na kukuta watu mbalimbali wakiwa katika hali ya majonzi sana. Mke wa Kamanda Ballow yuko Dar es Salaam na anatarajia kufika Mwanza.
 
Mpaka sasa Polisi wanamshikilia mtu mmoja aitwaye Dorcas kwa ajili ya Mahojiano huku uchunguzi mkali ukiendelea kuhusiana na kifo cha kamanda Liberetus Ballow.
PICHA NA HABARI NA B PLUS BLOG

No comments:

Post a Comment