Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Kapteni
Milton Lusajo Lazaro akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini D
ar es Salaam jana juu ya mpango wa shirika hilo kurejesha safari zake
kuanzia Ijumaa hii
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Kapteni
Milton Lusajo Lazaro (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari
jijini D ar es Salaam jana juu ya mpango wa shirika hilo kurejesha
safari zake kuanzia Ijumaa hii. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa
Shirika hilo Mwanamvua Ngocho
Baadhi
ya waandishi wa habari wakisikiliza malezo ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Kapteni Milton Lusajo Lazaro.
Picha na mpiga picha wetu.
====== ======== ======
ATCL yatangaza kuanzisha safari za ndani nyingine baada ya kurejesha huduma zake Ijumaa hii.
Na Mwandishi Wetu.
SHRIKA
la Ndege la Air Tanzania (ATCL) limejipanga kurudisha safari zake
Ijumaa hii na kuahidi kuongeza safari nyingine za ndani na za kimataifa
kupitia mpango wa Shirika hilo madhubuti unaolenga kurudisha heshima ya
shirika hilo.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu yashirika hilo
jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni
Milton Lusajo Lazaro alisema kuwa shirika lake limeanza kutekeleza
mpango wa maendeleo utakaosaidia kuboresha utoaji huduma pamoja na
upanuzi wa safari zake.
“Tumejipanga
kurejesha huduma zetu Ijumaa huku tukiwa tumepanga kuongeza safari
nyingine katika mkakati wetu wa kuhakikisha kuwa tunafika maeneo mengi
nchini. Tutaanza na safari ya Dar es Salaam-Mwanza-Kilimanjaro kabla ya
kuanzisha safari ya Dar es Salaam-Arusha-Zanzibar itakayozinduliwa
mwezi Novemba tarehe 2, 2012.
“Tunawashukuru
wateja wetu kwa kuwa nasi katika kipindi hichi kigumu tulipo simamisha
huduma zetu na tunaahidi kuwapatia huduma bora na za kipekee kipindi
tutakapoanza safari,” alisema Lazaro.
Lazaro
alisema kuwa shirika hilo la kitaifa pia lina mpango wa kuzindua safari
ya Dar es Salaam-Mtwara itakayoanza mwezi Novemba tarehe 16, 2012 kwa
kutumia ndege ya Dash 8-300 iliyokuwa katika matengenezo baada ya
kuhusika kwenye ajali kipindi kifupi kilichopita na badae kurejesha
safari zake za Dar-es Salaam- Hahaya(Moroni).
Hata
hivyo alisema kuwa shirika lina mpango wa kununua ndege mbili kubwa
zitakazotumika katika safari zake za kimataifa zinazotarajiwa kuanza
mnamo mwezi Desemba au mapema mwakani na kuzitaja safari za Dubai, China
na Ulaya kuwa miongoni mwa safari hizo.
“Sisi
ni shirika la ndege la taifa, tunahitaji kutunza heshima hii kwa kutoa
huduma zinazokidhi matakwa ya wateja wetu. Tumeweza kukabiliana na
changamoto mbalimbali na kupata suluhisho madhubuti. Kiukweli mara hii,
huduma zetu ni za kudumu.
“Changamoto
kubwa sasa ni kujikita katika urejeshaji wa heshima ya shirika.
Tumejipanga kununua ndege mbili mpya ili kupanua huduma zetu na wakati
mwingine tutaingia ubia na mashirika makubwa ya ndege ili kuongeza
safari zetu,” aliongeza.
Aidha,
akizungumzia kuhusu usitishwaji wa mkataba baina ya Kampuni ya ATCL na
kampuni ya Aero Vista mwezi Agosti ambayo iliwakodisha ndege aina ya
Boeing 737-500, Lusajo alisema kuwa mazungumzo baina ya kampuni hizo
mbili yanaendelea na kusema wanategemea kufikia makubaliano muda si
mrefu.
“Mazungumzo yanaendelea. Sitegemei kuwa tutafika pabaya. Najua tuu tufafika muaafaka,” alisema.
No comments:
Post a Comment